1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo yafanyika baina ya serikali nawapinzani nchini Misri

Abdu Said Mtullya6 Februari 2011

Mashirika ya habari yaripoti kuwa Makamu wa Rais wa Misri Omar Suleiman amekutana na wapinzani.

https://p.dw.com/p/10BXr
Makamu wa Rais wa Misri Omar Suleiman aliekutana na wapinzani.Picha: picture-alliance/dpa

Viongozi wengine wote wa ngazi za juu wa chama kinachotawala nchini Misri National Demokratic Party wamejiuzulu na kumwacha mwenyeketi wake Rais Hosni Mubarak.Waliojiuzulu ni pamoja na mtoto wa rais huyo Gamal Mubarak.

Katibu Mkuu mpya wa chama hicho sasa atakuwa bwana Hossam Badrawi anaesemekana kuwa na mtazamo wa kiliberali. Bwana Badrawi pia ana uhusiano mzuri na wapinzani wa serikali.

Wakati huo huo maandamano ya kumtaka Rais Mubarak aondoke madarakani mara moja yameendelea kwa amani nchini Misri kote.Na shirika la habari la AFP limeripoti kwamba chama cha Udugu wa Kiislamu kimeanza mazungumzo na viongozi wa serikali ya Misri ili kouna ni kwa kiasi gani serikali hiyo ipo tayari kuyakubali matakwa ya wananchi.

Kwa mujibu wa AFP,kiongozi mmoja wa Udugu wa Kiislamu amesema kuwa mazungumzo yalifanyika jana baina ya wajumbe wa chama chake na Makamu wa Rais mpya bwana Omar Suleiman.