1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbali na machafuko yanayoikabili, Serikali ya Sudan yafanya sensa ya kuhesabu watu.

Scholastica Mazula22 Aprili 2008

Serikali ya Sudan kwa mara ya kwanza imemaliza sensa ya kuhesabu watu kuwahi kufanyika katika kipindi cha miaka kumi na tano ambayo ni historia.

https://p.dw.com/p/Dmp5
Rais Omar el-Bashir wa SudanPicha: AP

Hatua hii inafuatia makubaliano ya amani yaliyokomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mrefu zaidi barani Afrika.

Hata hivyo inaweka kiwingu cha mzozo unaotishia kuzidi kudhoofisha zaidi makubaliano hayo ya amani.

Katika makubaliano yaliyotiwa saini mwaka 2005 na makundi ya zamani yaliyokuwa yakipigana Mashariki na Kusini mwa nchi hiyo, sensa hiyo ya watu ni ya muhimu sana kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kuweka ulingano wa utajiri na kushirikiana madaraka katika Serikali hiyo ya Afrika ya Kati.

Lakini upande usiokuwa na maendeleo wa Kusini mwa nchi hiyo umekataa kulazimishwa kukubali matokeo ya sensa hiyo na Waasi katika jimbo la Darfur watagoma kuhesabiwa.

Pande zote mbili zinaushutumu upande wa Mashariki wenye waarabu wengi kwa kuendesha sensa hiyo ya kuhesabu watu kibinafsi kwa kuongeza utawala wake na kutaka kuwanyonya zaidi jamii ya Waafrika.

Serikali ya Khartoum ambayo kwa kiwango kikubwa imesaidiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa, imesema imetayarisha mkakati bora zaidi wa kuendesha zoezi la kuhesabu watu ambao haujawahi kutokea nchini Sudan tangu nchi hiyo ijipatie Uhuru wake kutoka kwa Mwingereza mnamo mwaka 1956.

Mkurugenzi wa ofisi ya Takwimu, Yasin Haj Abdin, anasema kwamba mipango na zoezi la kuhesabu watu katika eneo la Kusini linawezekana kwasababu kuna watu wa kuhesabu katika eneo hilo na kuna mbinu za Kimataifa ambazo zitawasaidia kupata idadi kamili ya watu.

Kuna idadi ya watu sitini elfu wanao hesabu kura wakiwa chini ya waangalizi miambili na watahesabu kiasi cha watu wanaokadiriwa kufikia milioni arobaini, kazi inayokadiliwa kuigharimu Sudan na jumuiya za Kimataifa kiasi cha dola milioni mia moja na tatu.

Pamoja na mvua kubwa iliyonyesha mjini Khartoum jana na sehemu nyingine za nchi hiyo na kusababisha katizo la Umeme, lakini zoezi la kuhesabu sensa ya watu lilianza kwa muda uliopangwa.

Mkuu wa Kamati ya uangalizi wa zoezi hilo, Abdel Bagi Gailani ameliambia Shirikala la Habari la Ufaransa kwamba wamepata matatizo kidogo kutokana na hali ya hewa kuwa niya mvua kila sehemu lakini wameendelea na kunaonyesha mafanikio zaidi.

Mapema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, alionya kwamba kucheleweshwa kwa zoezi hilo la kuhesabu watu kunapaswa kuzingatia pia masuala ya Kisiasa na matatizo ya Kiuchumi ikiwa ni pamoja na uchaguzi ujao.

Kundi la Kimataifa linaloshughulikia migogoro nalo tayari yameonya kwamba ratiba ya uchaguzi wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwakani iko nyuma sana kuliko vile ilivyokuwa imepangwa na kwamba matatizo ya huko Darfur yatahitaji mpango madhubuti au ratiba kamili ya uchaguzi itayarishwe upya.