1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MBANGA-PONGO:Watu wote 114 waliokuwa kwenye ndege ya Kq wathibitishwa kufariki

7 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC48

Wachunguzi wameanza kazi yao ya kuchunguzas kuhusu chanzo cha ajali ya ndege ya shirika la ndege la Kenya iliyoanguka huko Cameroon na kuua watu wote 114.

Luc Ndjodo mshtaki mkuu wa serikali ya Cameroon amesema waokoaji wameshapata miili kadhaa ya watu ikiwa ni zaidi ya saa 48 baada ya ndege hiyo aina ya Boeing 737-800 kutoweka kwenye mitambo ya rada na kuanguka.

Waziri wa uchukuzi wa Kenya Ali Chirau Mwakwere amethibitisha juu ya kutokuwepo manusura katika ajali hiyo.

Mabaki ya ndege hiyo yalipatikana kilomita 20 kutoka uwanja wa ndege wa Duala kusini mwa Cameroon.Shughuli za kutafuta maiti zinaendelea kufanyika chini ya ulinzi mkali wa polisi na helikopta.