1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbunge Halima Mdee akamatwa na polisi

5 Julai 2017

Ni baada ya mbunge huyo katika mkutano na waandishi wa habari kupinga tangazo la Magufuli kukataza wenye mimba kuendelea na shule. Mdee alisema Rais amefanya uamuzi wa "hovyo", maneno yanayochukuliwa kama kashfa.

https://p.dw.com/p/2fwrM
Mbunge wa CHADEMA Tanzania, Halima Mdee
Picha: DW/E.Boniface

J2 05.07 Tanzania - MP Mdee´s arrest - MP3-Stereo

Kamata kamata dhidi ya viongozi wa upinzani inaendelea kuripotiwa na kisa cha  karibuni kabisa ni kumatawa jana  kwa mbunge wa Kawe, jijini Dar es Salaam, Halima Mdee, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendelea, BAWACHA. Haya yanakuja katika wakati ambapo wabunge wengine watano wa chama hicho walitazamiwa kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumshambulia mwenzao wa chama tawala, CCM. Mohammed Abdul-Rahman amezungumza na mwandishi mkongwe wa habari na mchambuzi wa siasa za Tanzania, Salim Said Salim, kupata tathmini yake juu ya hiki kinachoendelea sasa na mustakabali.