1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mchango wa Ujerumani:

16 Julai 2008

Ujerumani kupitia jasusi wa BND iliandaa mpango wa kubadilishana wafungwa kati ya Israel na Hizbollah.

https://p.dw.com/p/Edf5

Mpango wa jana wa kubadilishana wafungwa kati ya Israel na Hizbollah nchini Lebanon,ulitokana na upatanishi wa Ujerumani.Miaka 2 barabara ,tangu kumalizika vita vya Lebanon, Hizbollah ilikabidhi maiti za wanajeshi wawili wa Israel.Kunyakuliwa kwa Ehud Goldwasser na Eldad Regeb Julai 12, 2006 na wanamgambo wa Hizbollah, ndiko kulikochochea vita vile vya Lebanon.

Sasa kusubiri kujua hatima yao kwa ukoo wa wanajeshi hao 2 kumemalizika.

Kwa ukoo wa wanajeshi Goldwasser na Regev,miaka hii 2 ya kutojua hatima yao ilikua ya mateso makubwa.Miaka 2 wakiomba salama kwa vipenzi vyao Udi na Eldad ambao walichukuliwa mateka na wapiganaji wa hizbollah hadi nchini Lebanon.

Familia hizo mbili zilifunga safari mnamo miaka 2 iliopita kwenda kila pembe ya dunia wakiwaomba viongozi wa dola na serikali kusaidia .Walizungumza hata na Baba mtakatifu na hata Katibu mkuu wa UM wakidai kuachwa huru kwa vijana wao ambao tangu siku ya kunyakuliwa kwao hawakupata habari zao. Madaktari wa Kiisrael na wataalamu wa kufuata nyayo za uhalifu waliojionea alama za damu pale Hizbollah ilipowavamia

vijana hao 2 wakati wakishika zamu na kupanga upya jinsi hujuma hiyo ilivyofanyika katika gari la aina ya jeep,waligundua tangu miaka 2 nyuma kuwa waliuwawa wakati waliposhambuliwa.

Vita ilivyofanya Israel ili kuwakomboa havikuhitajika.

Na mwishoe,israel ilipaswa kuungama na kulipa gharama kubwa.Ilipasa kumuacha huru gaidi alieua waisraeli 5 na wafungwa wengine 4 wa vita ili kurejeshewa maiti ya wanajeshi wake 2 pamoja na maiti nyengine za wanajeshi wake waliofariki vitani.

Uchungu mkubwa zaidi anauona hivi sasa Noam na Aviva Shalit.Mwanawe Gilad hata kabla ya vita vya Lebanon, alitekwanyara na wanamgambo wa kipalestina na kukokotwa hadi mwambao wa Gaza.Amedhibitiwa huko miaka 2 sasa.

Hivi sasa ametimiza miaka 21 na mwisho wa kizuizi chake hauonekani.

Kwa upande wapili,kuna maalfu ya wafungwa wa kipalestina katika magereza ya Israel na kati yao ni chipukizi na wale ambao wamezuwiliwa hata bila mashtaka yoyote na bila hukumu zozote.

Uchungu na majonzi yao hakuna anaezungumza.Ni pale wafungwa wa aina hii miongoni mwao wabunge waliochaguliwa wa kipalestina wakiachwa huru na Gilad Shalit akirejea nyumbani na kuanza maisha mapya, ndipo ukurasa mpya unaweza kufunguliwa Mashariki ya kati.

Hatahivyo, siku hizi za msiba na huzuni zimetoa shujaa wake: mpatanishi wa kijerumani Gerhard Conrad ambae kwa ujanja na busara nyingi na hata subira kubwa ,afisa huyo wa BND-idara ya Usalama ya Ujerumani,ameandaa mpango wa jana wa kubadilishana wafungwa na amebaki chini kwa chini haonekani hadharani .Anastahiki kupewa heko.

Ametenda mengi,kwani ameonesha dhamana ya Ujerumani kwa taifa la israel ambayo inasisitizwa tena na tena na serikali ya Ujerumani,sio lazima imelengwa dhidi ya masilahi ya nchi jirani za kiarabu.Kwa ni jasusi wa kijerumani ameibuka mpatanishi asieelemea upande wowote na kukubalika,yabainisha Ujerumani hivi sasa inatoa sura nyengine kabisa Mashariki ya kati-sura ya kujikwamua kutoka hisia za madhambi yaliopita na kutumikia masilahi tangu ya Israel hata ya jirani zake wa kiarabu.