1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mchezaji mpira akataa kucheza Israel

P.Martin10 Oktoba 2007

Mchezaji mpira Ashkan Dejagah wa timu ya Ujerumani ya vijana walio chini ya umri wa miaka 21 amesema,yeye hatoshiriki katika mchezo wa siku ya Ijumaa nchini Israel.Sababu iliyotolewa na mchezaji mpira huyo mwenye asili ya Kiirani ni uhusiano wa mivutano kati ya Iran na Israel. Serikali ya Iran inazuia wanaspoti wake kushiriki katika mashindano na Israel.

https://p.dw.com/p/C7iE

Ashkan Dejagah alie na uraia wa Ujerumani na Iran amesema,sababu za binafsi na kisiasa zinamzuia kushiriki katika mchezo wa siku ya Ijumaa utakaochezwa Israel.Sasa,wanasiasa wa Kijerumani wa vyama vya CDU na SPD wanauliza:Tutaishia wapi ikiwa wanaspoti wataamua watacheza dhidi ya nani? Spoti haipaswi kuchanganywa na siasa.Hoja hiyo imetolewa na wale wanaotenda hilo.

Baraza Kuu la Wayahudi nchini Ujerumani linasema;haiwezekani kwa mchezaji wa timu ya taifa kuanzisha kitendo cha binafsi kususia Uyahudi.

Ni dhahiri kuwa mhamiaji alieomba uraia wa Kijerumani anapaswa kujaribu kuwa sehemu ya jamii ya Kijerumani.Lakini hiyo haimaanishi kuwa anapopata uraia mpya,anasalim kila kitu kilichohusika na maisha yake ya zamani ikiwa ni pamoja na kule alikotokea.Bila ya shaka atakuwa na uhusiano na nyumbani kwake,ana ndugu na rafiki na hata mali.Ikiwa Mjerumani asili anaweza kuwa na uhusiano wa kibinafsi na nchi ya kigeni, kwanini mhamiaji pia asiwe na uhusiano wa aina hiyo na kule alikotokea?

Haitokuwa haki au sawa kudai jingine kwa mhamiaji,na mara nyingi hali hiyo inaheshimiwa ila siasa inapoingia kati.Na hiyo ndio hali ilivyo kuhusu Iran na Israel.Si kwa sababu mchezaji mpira Dejagah anataka kuchanganya mambo hayo mawili.Wanaowajibika wapo Teheran na Jerusalem na wanasababisha uhasama kati yao. Lakini anaeumia ni mtu wa kawaida kama ilivyo kesi ya mcheza mpira huyu anaekabiliwa na mzozo mkubwa na kitisho cha kuadhibiwa.

Kwa hivyo,itakuwa busara ikiwa vyombo vya habari vya Ujerumani na hata wanasiasa hawatolifanya suala hilo kuwa kubwa sana.Kwani angekuwepo mchezaji mpira wa Kijerumani,asili ya Kiyahudi katika timu ya taifa ya Ujerumani ya vijana chini ya umri wa miaka 21 na mchezo ungechezwa Iran, basi ni wazi kuwa mchezaji huyo asingeshikiliwa kushiriki katika mchezo huo.

Hapo ujumuishaji katika jamii una sura mbili:Wale wanaojijumuisha na wale wanaokubaliwa na jamii au wasiokubaliwa.Kujijumuisha katika jamii haimaanishi mtu kukanusha asili yake bali panahitajika hali ya kuvumiliana,kuthaminiana na kuheshimiana kutoka kila upande.Katika kadhia ya mchezaji mpira Dejagah,hayo yote yanakosekana.