1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mchezo wa kuigiza Ugiriki wafikia mwisho kura ya maoni hakuna

4 Novemba 2011

Mahesabu ya waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreou yameparaganyika. Kwa kutaka kuitisha kura ya maoni alitaka kuwatwika wananchi jukumu, la kutoa maoni yao pamoja na kuunga mkono msaada kwa nchi yao

https://p.dw.com/p/134vh
Waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreou akiondoka kutoka mjini Cannes ambako kunafanyika mkutano wa G20.Picha: dapd

Mahesabu ya waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreou, yameparaganyika. Kwa kutaka kuitisha kura ya maoni alitaka kuwatwika wananchi jukumu, la kutoa maoni yao pamoja na kuunga mkono moja kwa moja mpango wa msaada wa kimataifa. Akijikuta katika upinzani mkubwa kutoka upande wa vyama vya upinzani pamoja na baadhi ya wajumbe wa chama chake tawala cha Pasok dhidi ya hatua za kubana matumizi, amejaribu Papandreou kufanya lolote linalowezekana kurekebisha hali hiyo.Amejitoa katika malumbano ya kisiasa na kuwageukia wananchi kuhusu suala hili.

Amesahau lakini kuwa , Ugiriki si tu kwamba ni nchi yenye madeni , lakini pia unafilisika. Katika hali hii kitu muhimu ni uchumi na sio siasa. papandreou ameyaweka masoko katika hali isiyokuwa thabiti pamoja na washirika wake wa Ulaya , na ametambua katika mkutano wake mfupi na kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa mjini Cannes kuwa amepuuzwa. Katika muda wa saa 48 alibidi kubadilisha kauli yake ya kuitisha kura ya maoni . Bila hivyo msaada wote kwa Ugiriki ungesitishwa.

Ugiriki inahitaji kiwango fulani cha msimamo wa pamoja baina ya vyama vikubwa vya kisiasa , yaani chama tawala cha Pasok pamoja na kile cha kihafidhina cha New Democratic. Ni kwa njia hiyo tu ambapo itawezekana kuzitekeleza hatua ngumu lakini za lazima. Na pia jana Alhamis kulipatikana ishara ya kwanza kuelekea katika njia sahihi kwa upande wa chama cha Democratic. Mwenyekiti wake Antonis Samaras alitangaza kuwa makubaliano yaliyopatikana katika mkutano wa umoja wa ulaya hapo Oktoba 27 kuhusu kupunguza deni la Ugiriki kwa asilimia 50, atayaunga mkono bungeni , hata kama kutakuwa na serikali ya umoja wa kitaifa.

Griechenland Finanzkrise Opposition Antonis Samaras Partei Neue Demokratie
Kiongozi wa chama cha upinzani cha kihafidhina nchini Ugiriki Antonis Samaras.Picha: dapd

Masoko yamejisikia ahueni na serikali za Ulaya zimejisikia kuwa na matumaini tena. Je nguvu hii ya kidemokrasia , inaweza kutumiwa na nchi nyingine zenye madeni wanachama wa umoja wa sarafu ya euro kama Ureno na Ireland. Inawezekana hatimaye hata Ugiriki vyama vikuu sasa vikafanyakazi kwa pamoja , ili kuweza kuiokoa nchi yao kupitia nguvu zao binafsi?.

Hali ya matumaini makubwa ilionekana hata hivyo. Ilionekana kuwa Samaras alikuwa anafikiria kuwa papandreou atatangaza kujiuzulu mara moja, na kuundwa serikali ya mpito na uchaguzi ufanyike katika muda wa wiki sita. Inaonekana kuwa mbali ya uungwaji mkono na chama chake katika kura ya kuwa na imani bungeni leo lakini uungwaji wake mkono ni mwembamba.

Mwandishi : Moskovou, Spiros / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Mohammed Khelef.