1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Ugaidi

Mchungaji Paul Mackenzie afikishwa mahakamani Mombasa

Amina Mjahid
23 Januari 2024

Mhubiri wa kanisa la Good News International, Paul Mackenzie na wenzake 94 hii leo wanafikishwa katika Mahakama Kuu ya Mombasa nchini Kenya kusomewa mashtaka ya jinai.

https://p.dw.com/p/4bbFQ
Kenya Kilifi | Ufukuaji wa miili ya wafuasi wa kundi la kidini nchini Kenya
Watu zaidi ya 400 waliripotiwa kuuawa kwa kuamriwa na mchungaji Mackenzi kujinyima chakua ili wakutane na Yesu.Picha: Stringer/REUTERS

Watu hao 95 wameshtakiwa kwa makosa ya mauaji.

Siku ya Alhamisi wiki hii Mackenzie na washukiwa wenzake watafikishwa katika mahakama ya watoto ya Tononoka mjini Mombasa kusomewa mashtaka mengine ya dhulma na mauaji ya watoto yaliyotekelezwa huko Shakahola.

Soma pia: Paul Mackenzie kufunguliwa mashtaka ya mauaji na ugaidi

Watuhumiwa hao pia wanatarajiwa kushtakiwa kwa makosa ya kukiuka haki ya elimu ya watoto kinyume na sheria.

Alhamis wiki iliyopita, Mackenzie na wenzake walikanusha mashtaka ya ugaidi waliyofunguliwa katika mahakama moja ya mjini Malindi, baada ya amri ya mahakama hiyo kwamba ingewaachia huru iwapo mashtaka dhidi yao hayangefunguliwa katika kipindi cha siku 14.