1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mda wa kikosi cha kimaitaifa kikiongozwa na Marekani nchini Iraq umeongezwa hadi mwaka 2008

Siraj Kalyango19 Desemba 2007

Lakini jeshi la Marekani litabaki huko hata baada ya 2008

https://p.dw.com/p/Cdoc
Ngege za kivita za Marekani aina ya F-16 zikishika doria katika anga ya Iraq kama sehemu ya jeshi la kimataifa la Iraq. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limerefusha mda wake huko hadi 2008.Picha: AP

Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa limerefusha mda wa kikosi cha kimataifa nchini Iraq-MNF- kinachoongozwa na Marekani wa kuendelea kukaa nchini Iraq hadi mwisho wa mwaka wa 2008.

Baraza la wanachama 15 limeidhinisha pendekezo la kifungu nambari 1790, kinachokubali kikosi cha kimataifa kikiongosi hicho kuendelea kubaki huko hadi Disemba 31 mwaka wa 2008, baada ya kuombwa na serikali ya Iraq.

Lakini majeshi ya Marekani yatabaki nchini Iraq hata baada ya mwaka w a 2008,hata hivyo utawala wa Baghdad, unayataka yawekwe chini ya mkataba wa nchi hizo mbili yaani Iraq na Marekani badala ya ule wa unaozihusisha nchi kadhaa.

Pendekezo hilo pia linakipengele kinachotoa idhini kwa serikali ya Iraq kufupisha mda huo ikipenda.

Katika barua alioiandikia baraza hilo akiomba kurefushwa kwa mda huo,Waziri mkuu wa Iraq, Nuri al-Maliki, amebaini kuwa kikosi cha majeshi ya kimataifa-MNF-kimetoa mchango muhimu kusaidia shughuli za kurejesha usalama pamoja na utawala wa sheria katika nchi hiyo ambayo imezongwa na ghasia.

Pia kikosi hicho kimesaidia kuimarisha ujenzi wa jeshi la taifa pamoja na vikosi vingine vya usalama.

Maliki amesema kuwa vikosi vya usalama vya nchi yake sasa vimechukua jukumu la ulinzi wa mikoa nane kutoka kwa kikosi cha kimataifa cha -MNF.Aidha amesema anataraji kuwa hii ndio itakuwa mara ya mwisho ya serikali kuomba umoja wa Mataifa-kurefusha zaidi mda wa kikosi cha MNF kubaki huko.malik anategemea kuwa mda hautakuwa mrefu ambapo vikosi vyake vitakuwa na uwezo wa kudhibiti hali ya usalama katika mikoa yote 18 ifikapo mwaka wa 2008.

Na katika barua tofauti kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa- waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani,Condoleezza Rice, ameahidi kuwa kikosi cha MNF kiko tayari kutekeleza vilivyo kazi kitakachopewa.

Idhini ya kurefusha kikosi cha kimataifa nchini Iraq, imekuja wakati Marekani kuilaumu Iran kwa kuendelea kuwapa silaha wapiganaji wa chini kwa chini wa Kishia wa Iraq licha ya ahadi ya rais Ahmed nejad ya kuwa atasaidia kukomesha mtiririko wa silaha kwa wapiganaji hao.

Ripoti ya Pentagon yenye kurasa 60, inasema kuwa majeshi ya Marekani yamefaulu kupata 'maendeleo ya kiusalama' katika kipindi cha miezi mitatu iliopita. Imeendelea kuwa mashambulizi yamepungua kwa asili mia 62 tangu machi.Mashambulizi ya mabomu ya motokaa ya kila wiki yamepungua kufikia 600 kati ya mwezi Oktoba kutoka 900 mwezi wa Septemba.Lakini katika mwezi wa Juni mashambulizi yalikuwa yanafikia 1,600 kwa wiki.

Hata hivyo ripoti inasema kuwa kunahitajika maridhiano ya kitaifa ili kuweza kupata maendeleo ya mda mrefu.Kuhusu mdaa wa silaha kutoka Iran, ripoti inasema mambo hayajabadilika kuhusiana kuyafadhili na kuyapa mafunzo makundi haramu ya wapiganaji wa Kishia wa Iraq.

Kwa mda huohuo, waziri mkuu mpya wa Poland Donard Tusk amefanya ziara isiyotarajiwa nchini Iraq,akiwa na ujumbe wa Krismasi kwa askari 900 wa Poland walioko kusini mwa Baghdad.Jumanne utawala wake ulimuomba rais Lech Kaczynski kuongezea mda wa askari wake walioko Iraq hadi Oktoba mwaka ujao wa 2008.Inataegemewa rais atakubali ombi hilo. Kisheria mda wa askari hao unamalizika mwisho wa mwaka huu.