1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Medvdev akaribishwa kama mwanasiasa wa sera za wastani

11 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZyZ

Serikali ya Ujerumani imekaribisha uteuzi wa Dmitri Medvedev kama mrithi wa Rais Vladimir Putin wa Urusi.Waziri-Mdogo katika Wizara ya Masuala ya Nje ya Ujerumani,Gernot Erler amesema, kuteuliwa kwa Medvedev kunaimarisha kambi ya kiraia nchini Urusi kwani mwanasiasa huyo hatoki idara ya upelelezi wala jeshini na amejitokeza kama mwanasiasa mwenye sera za wastani.

Medvedev alie na umri wa miaka 42,ni mwenyekiti wa kampuni kubwa ya mafuta nchini Urusi-Gazprom na ni mshirika mkuu wa Putin tangu miaka 17 iliyopita na aliongoza kampeni za Putin wakati wa uchaguzi hapo mwaka 2000.Katiba ya Urusi haimruhusu Putin kugombea tena wadhifa wa rais.