1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mehari Tedali,Ethiopia

23 Mei 2013

Muethiopia huyu ni mtafiti katika taasisi ya taaluma za usalama katika mji mkuu Addis Ababa. Huko pia ndiko yanakokutikana makao makuu ya Umoja wa Afrika.

https://p.dw.com/p/18cAi
Das Bild zeigt Dr. Mehari Tadele, wurde in Addis Abeba, Äthiopien, aufgenommen, von Yohannes G/egziabher, DW-Korrespondent der Amharisch-Redaktion. Zulieferer: Friederike Müller
50 Jahre Afrikanische UnionPicha: DW/Y. Gegziabher

"Changamoto zilizoko hivi sasa ni jinsi ya kusonga mbele toka enzi za kuingilia kati na ukombozi na kuingia katika enzi za kidemokrasia ambapo ahadi zinazotolewa zitatekelezwa kikamailifu. Kipaumbele hapo ni majukumu na michango ya Umoja wa Afrika, demokrasia na masuala chungu nzima, kwa jumla: sababu zenyewe hasa za matatizo mengi ya kisiasa barani Afrika. Tutaraji Umoja wa Afrika utayashughulikia matatizo hayo mnamo wakati huu wa kuadhimisha miaka 50 tangu ulipoanzishwa."