1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mei Mosi, siku hii inaumuhimu gani kwa wafanyakazi.

Sekione Kitojo30 Aprili 2007

Siku ya wafanyakazi duniani, inaitwa Mei mosi duniani kote. Kwa wafanyakazi watu wazima hadi sasa wanajiweka katika vyama vyao vya wafanyakazi, wanajikusanya katika siku hii ili kufanya kumbukumbu. Lakini hivi sasa idadi ya wanachama wa vyama hivi vya wafanyakazi inazidi kupungua kwa kasi kila mwaka. Hapa unabadilika ulimwengu wa kazi kwa kasi kubwa kwani mishahara na mapato vinapaswa kuwa katika hali ya uhakika zaidi kama ilivyo nafasi za kazi.

https://p.dw.com/p/CHFD

Kiasi cha wafanyakazi 100 wa kampuni la bima la Allianz, walijikusanya katika eneo la ndani la mji wa Koln. Mama Allianz anawatupa wanawe, ilikuwa inaonekana wazi. Wengi wa waandamanaji wakiwa wanapepea bendera nyekundu ya chama cha wafanyakazi cha VERDI. Wakati wafanyakazi hao wa shirika la Allianz kwa muda wa mwaka mmoja walifahamu kuwa shirika lao linapunguza nafasi za kazi 7,500. wamebaki wakishangaa. Hakuna mfanyakazi ambaye ana bima nchini Ujerumani atakuwa na wasi wasi katika nafasi yake ya kazi. Nafasi ya kazi katika eneo hili inakwenda kiasi cha zaidi ya muongo mmoja kama kazi yenye malipo mazuri kwa maisha yako yote.

Binafsi niko na Allianz kwa muda wa miaka 30, na wakati fulani nimekuwa kwa kweli najivunia sana, kwamba kama mfanyakazi nimekuwa nikitendewa vizuri kabisa, pamoja na mafanikio . na kwamba tuko katika kazi ambayo inahusu binadamu. Hiyo sasa haipo tena.

Na kwa hiyo Gbriele Burghard-Berg na wafanyakazi wenzake kwa mara ya kwanza katika maisha yao wanapaswa kupambana ili kulinda kazi zao, wanapaswa pia kujiunga na maandamano ya vyama vya wafanyakazi wa Ujerumani na kupepea bendera zao. Na kwake yeye chama cha wafanyakazi kwa mara ya kwanza kinakuwa ni chanzo cha matumaini. Kwa karibu mwaka mmoja kabla ,asilimia 15 ya wafanyakazi wote wa shirika hilo la bima walikuwa wanachama wa chama hicho cha wafanyakazi cha VERDI.

Na kuanzia wakati huo ni wazi kwamba kutokana na upunguzaji wa nafasi za kazi katika shirika la Allianz, chama hicho cha wafanyakazi kinapata wanachama wapya kila siku. Hatua ambayo inaonekana pia katika maeneo mengine, anasema Wolfgang Uellenberg. Yeye ni mkuu wa vyama vya wafanyakazi vya majimbo, chama ambacho ni chama mama cha vyama vya wafanyakazi nchini Ujerumani.

Katika wakati huo , ambapo watu wamegundua kwamba inahusu fedha yao , inahusu nafasi zao za kazi, wanajiunga nasi. Kwa hiyo tunahitaji kinga, tena tunahitaji sauti ya pamoja, ya kule tunakokwenda. Tunafahamu pia kuwa tunapoteza wanachama kutokana na wanachama wazee, ukosefu wa kazi, lakini tunapata wanachama kupitia wanachama vijana , wanawake na kile kinachoitwa, wafanyakazi kwa jumla, kwa wale wanaofanyakazi muda wote kwa kuwa watu wanasema , ndio niko katika hatari, siwezi kujitokeza mimi peke yangu, na chama cha wafanyakazi kiko kwa ajili yangu.

Kwa kurudi tena kwa muungano wa vyama maandamano ya Mei Mosi katika eneo la Alexanderplatz yanafika mwisho.

Na siku ya wafanyakazi inakuwa tu kwa vyama vya wafanyakazi. Hata hivyo pamoja na kupunguza nafasi za kazi katika mashirika ya bima, beni ama shirika la simu kila wakati wanachama wanapungua. Wolfgang Uellenberg kutoka chama cha wafanyakazi cha DGB anafahamu, kuwa yeye pamoja na wanachama wenzake hawezi kuzuwia mabadiliko haya na kwamba wengi watajiunga na maandamano ya hapo Mei mosi na kupata bia moja pamoja na kufurahia sherehe ambazo zinaambatana na kuwapo na watu kadha tu.