1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meja Bernard Ntuyahaga aliyekuwa afisa wa jeshi la Rwanda ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

6 Julai 2007

Mahakama ya Ubelgiji imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela aliyekuwa afisa wa jeshi la Rwanda Meja Bernard Ntuyahaga baada ya kumkuta na hatia ya kuhusika na mauaji ya wanajeshi 10 wa Ubelgiji wa kulinda amani katika kipindi cha mwanzo cha mauaji ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

https://p.dw.com/p/CHBV
Hata hivyo mahakama haikumkuta na hatia ya kuhusika na mauaji ya aliyekuwa na hatia ya kuhusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Rwanda wakati huo bibi Agathe Uwilingiyimana.Bwana Bernard anaweza kukata rufaa kupinga hukumu hiyo. Lakini hukumu iliyopitishwa imewapa hisia gani wanaoshughulikia suala la mauaji ya Rwanda.
Saumu Mwasimba amezungumza na balozi wa Rwanda katika mahakama inayohusika na kesi hiyo ya Arusha bwana aloys Mutabingwa naye alikuwa na haya ya kusema.