1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meli ya abiria yapinduka; nahodha awekwa korokoroni

Sekione Kitojo15 Januari 2012

Nahodha wa meli ya abiria atiwa korokoroni nchini Italia ,huku uchunguzi ukifanyika juu ya madai ya kuuwa bila kukusudia.

https://p.dw.com/p/13jry
epa03059552 The Costa Concordia cruise ship is pictured listing just off the island of Giglio, northern Italy, early 14 January 2012, after she ran ground in the early hours of the morning. At least 50 people were believed to be missing after the cruise ship ran aground off Italy's western coast and began to sink, media reported 14 January. The Costa Concordia liner had set off on 13 January from the port of Civitavecchia, near Rome, for the start of a Mediterranean cruise, when its crew signalled an electrical fault to port authorities. EPA/MAURIZIO DEGL'INNOCENTI
Meli ya abiria Costa Concordia ambayo inaendelea kuzamaPicha: picture-alliance/dpa

Vyombo vya habari nchini Italia vimeripoti jana kuwa nahodha wa meli ya abiria , inayojulikana kama Costa Concordia , ambayo ilipinduka katika pwani ya Toscana , nchini Italia, ikiwa na abiria 4,000 amekamatwa wakati uchunguzi unafanyika juu ya madai ya kuuwa bila kukusudia na kuitelekeza meli yake.

Meli hiyo ya abiria iligonga mwamba baharini na kusababisha tundu la mita 70 hadi 100 katika eneo lake la mbele , muda mfupi baada ya kuanza safari siku ya Ijumaa kutoka bandari ya Civitavecchia karibu na Rome. Kiasi ya watu 42 wamejeruhiwa , ambao watu wawili hali zao ni mbaya na wengine 41 ambao ni miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya meli hiyo wakiwa hawajulikani waliko. Meli hiyo ilikuwa ikielekea katika bandari ya Savona kaskazini-magharibi ya Italia na ilitarajiwa kusimama katika bandari za Marseille nchini Ufaransa pamoja na Barcelona nchini Hispania.