1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meli ya kontena ya kijerumani yaachiwa.

4 Agosti 2009

Maharamia wa kisomalii wamelipwa fidia

https://p.dw.com/p/J3Wb

►Ile melii ya kijerumani inayopakia shehena iliotekwanyara miezi 4 iliopita iitwayo "HANSA STAVANGER" sasa imeachiwa na maharamiia wa kisomali ili kuendelea na safari yake .Msemaji wa kikosi cha Umoja wa ulaya "EU-OPERATION-ATLANTA", aliarifu mjini Nairobi, kuwa baada ya kulipwa fidia ya kiasi cha dala milionii 3 jana jioni , meli hiyo shirika la Leonhard na Blumberg mjinii hamburg,imengoa nanga kutoka pwani ya Somalia ya Haradhere na imeelekea upande wa kaskazini.

Meli hiyo inayopakiia makontena ilitiiwa nguvuni mwanzoni mwa April bahariini kati ya pwani ya Kenya na visiwa vya Seyschelles.Ndani yake wamo mabaharia 4 wa kijerumani,warusii 3 waukraine 2 na wafilipino 14.

Kwa mabaharia 24 wa meli hiyo ya kijerumani-Hansa Stavanger" kipindi cha kutekwanyara kimemalizika.Maharamia wa kisomali ndani ya melii hiyo kwa muujiibu wa matamshi yao wenyewe ,wamepewa kitita cha Euro kiasi cha miilioni 2 ikiiwa fidia.Shiriika lenye kumiliki meli hiyo mjiini Hamburg,Ujerumani (Leonhard und Blumberg) halikutoa tamshi lolote hadi sasa.

Nahodha wa meli hiyo mjerumani wiki chache ziilizopta alielezea halii ya mabaharia wake ndani ya barua.Aliandika kwamba hawakuwa na chakula wala cha kunywa na sehemu kubwa ya mabaharia wake ni wagonjwa.

Wakati fulani kwa muujibu wa nahodha huyo, maharamia wakionesha ukatiili na wakiwapa mahabusu wao mtihani mkubwa wa kiakili.Mfano baadhi ya mabahariia wakiwatiia vitunga vya macho na kuwafyatulia pembeni risasi.

Baada ya kuitekanyara meli hiyo baharini kati ya Kenya na Seyschelles,maharamia hao wa kisomali waliiiongoza meli hiyo ya Hansa Stavanger karibu na bandarii ya Haradere ya Somalia -shina la harakati za uharamia wa kiisomali.Baadae maharamia zaidi wakajiunga na wale wa asili na ambao wakitaka sehemu yao ya fidia.Hii pia ilitatiza majadiiliano na kampuni la meli hiyo mjini hamburg kwaviile muda mfupi maafiikiano yakikaribia,kunajitokeza mjumbe mpya wa kujadiliana.Kuna wakati mabaharia wa meli hiyo waliletwa nchi kavu ili kudai fidia kwa kila mmoja wao.

Maharamia wa Kisomali wameweza kuchota vitiita vikubwa vya fedha mnamo miezi iliopita kutokana na uharamia.Hivi sasa bado meli darzenii 1 zimo mikononi mwao ziikiwa na jumla ya mabaharia 200.

Mwandishi:Diekhans Antje/WDR/Ramadhan Ali

Mhariri:M.Abdul-Rahman