1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

300812 China Merkel

Abdu Said Mtullya30 Agosti 2012

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amehudhuria kikao cha mashauriano baina ya serikali za Ujerumani na China mjini Beijing .Katika ziara hiyo ya sita nchini China, Kansela Merkel anafuatana na mawaziri wake saba

https://p.dw.com/p/160Kc
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akisalimiana na Waziri Mkuu wa China Wen Jiabao mjini Beijing
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akisalimiana na Waziri Mkuu wa China Wen Jiabao mjini BeijingPicha: dapd

China imesema ipo tayari kusaidia katika juhudi za kuutatua mgogoro wa madeni barani Ulaya.Waziri Mkuu wa China,Wen Jiabao aliyasema hayo baada ya mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Beijing. Waziri Mkuu wa China ameeleza kuwa nchi yake itaendelea kuzinunua hati za dhamana za nchi za Ulaya zilizolemewa na madeni na pia itaimarisha mashauriano na Benki Kuu ya Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa,IMF.

Wen Jiabao amesema mgogoro wa fedha duniani pamoja na mgogoro wa madeni barani Ulaya unaiathiri dunia kwa kiwango kikubwa.Amesema China na Ujerumani kama mataifa makubwa ya kiuchumi duniani na kama washirika wakubwa wanapaswa kujenga imani baina ya mataifa na kwa pamoja China na Ujerumani zizikabili changamoto na ziendelee na juhudi ili kuleta mustakabal wa uhakika duniani

Katika ziara yake nchini China Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anafuatana na mawaziri saba na wajasirimali 20.China na Ujerumani zimetiliana saini mikataba ya biashara thamani ya mabilioni. Pamoja na mikataba hiyo ni mauzo kwa China ya ndege 50 za abiria za kampuni ya Airbus.

Katika tamko juu ya kikao cha pili cha mashauriano baina ya serikali za Ujerumani na China nchi hizo zimesisitiza utayarifu wa keundeleza mdahalo juu ya utawala wa kisheria na haki za binadamu. Kansela wa Ujerumani amewataka viongozi wa China wahakikishe uhuru zaidi kwa waandishi wa habari kutoka nje.Amesema uhuru wa vyombo vya habari ndiyo msingi utakaoyawezesha mataifa ya Ujerumani na China yajuane vizuri zaidi."

Katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa China Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alilijadili na mwenyeji wake ,Waziri Mkuu Wen Jiabao, suala la haki za binadamu ingawa mitazamo inatafautiana juu ya suala hilo.

Baada ya kikao cha pili cha mashauriano baina ya serikali za Ujerumani na China pande mbili hizo zimetoa tamko la pamoja kusema kuwa nchi mbili hizo zinadhamiria kuimarisha mdahalo juu ya masuala ya fedha. Na kwa manufaa ya kuimarishan uchumi mabenki na kampuni za nchi hizo zisaidiwe katika biashara na uekezaji wa vitega uchumi.

Kuhusu biashara na uchumi, China na Ujerumani zimetiliana saini mikataba ya ushirikiano katika sekta za Uchumi,nishati,tiba,utafiti na ulinzi wa mazingira.

Mwandishi,Doris,Krannich

Tafisiri:Mtullya abdu.

Mhariri.Abdul.Rahman