1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel akitaka chama chake kifanye kampeni za nguvu

5 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXEe

HANOVER.Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekitaka Chama chake cha Christian Democtaric Union CDU kufanya kampeni za nguvu kwa ajili ya uchaguzi kwenye majimbo matatu hapo mwakani.

Aidha kiongozi wa chama cha Christian Social Union CSU ambacho ni chama shirika na CDU,Erwin Huber ametabiri ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2009.

Huber alitoa hotuba ya kufunga mkutano wa siku mbili wa chama cha CDU katika mji wa Hanover, ambapo chama hicho kimeendelea na msimamo wake wa kupinga Uturuki kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Ulaya na badala yake ipewe tu nafasi zaidi za kushirikiana na umoja huo.