1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel amaliza ziara yake Kenya

12 Julai 2011

Nchini Kenya, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, anaihitimisha ziara yake rasmi ya siku moja. Bibi Merkel aliwahutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi .

https://p.dw.com/p/11tjk
Kansela Angela Merkel na waziri mkuu Raila Odinga,katika mkutano na waandishi habariPicha: picture alliance/dpa

Nchini Kenya, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, anaihitimisha ziara yake rasmi ya siku moja. Bibi Merkel aliwahutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi na pia kukutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP, Achim Steiner. Azma na dhamira ya ziara hii rasmi ni kuuimarisha uhusiano na Kenya baada ya Ujerumani kuzindua sera mpya ya mkakati mpya ushirikiano na bara la Afrika hivi karibuni .