1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel anataka Uingereza imara ndani ya Umoja wa Ulaya

27 Februari 2014

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameliambia bunge la Uingereza leo(27.02.2014) kuwa hayuko tayari kuahidi mageuzi makubwa katika Umoja wa Ulaya kwa ajili tu ya matakwa ya Uingereza.

https://p.dw.com/p/1BH2S
Angela Merkel Besuch in London
Kansela Angela MerkelPicha: picture-alliance/dpa

Kansela Angela Merkel lakini amesema kundi hilo la mataifa linahitaji kufanya baadhi ya mageuzi na kwamba Uingereza inahitaji kubakia katika umoja huo.

Akiwa mjini London kwa ziara ya kihistoria ya siku moja wakati hali ya kuutatanisha juu ya hali ya baadaye ya Uingereza katika Umoja wa Ulaya inaongezeka kwasababu ya ahadi ya kura ya maoni aliyotoa waziri mkuu David Cameron kwa Waingereza ya kubakia ama kuondoka katika umoja huo, Merkel ameshauri kuwa yuko tayari kwenda umbali lakini sio wote, kuweza kutimiza baadhi ya madai ya waziri mkuu Cameron.

Merkel und Cameron kommen sich näher
Waziri mkuu David Cameron akisalimiana na kansela Angela MerkelPicha: Reuters

Baadhi wanatarajia kuwa hotuba yangu itafungua njia kwa ajili ya mageuzi muhimu katika sura ya Ulaya ambayo itakidhi aina zote za matumaini yanayofikiriwa ama yale halisi ya Waingereza. Nasikitika kuwa hayo hayatatokea.

Merkel ameongeza kuwa wengine wanatarajia kitu tofauti kabisa na wanataraji kuwa nitatoa ujumbe wa wazi na mwepesi hapa mjini London kuwa Ulaya nzima haiko tayari kutoa gharama yoyote kuibakiza Uingereza katika Umoja wa Ulaya. Nasikitika kuwa matumaini haya hayapo.

Badala yake , Merkel ameashiria kuwa ataunga mkono nia ya Cameron ya kuzuwia uendeaji kinyume sheria ya uhuru wa kwenda kokote utakako katika Umoja wa ulaya wakati ikija katika suala la mafao ya kijamii, hususan ataunga mkono msukumo wake wa udhibiti wa halmashauri ya Umoja wa ulaya, na kwamba Uingereza itakuwa na nafasi, pamoja na mataifa mengine, kuwasilisha mapendekezo ya mageuzi wakati ujumuisho wa eneo la euro utakapotokea.

David Cameron in Peking
David CameronPicha: Getty Images

Akiwahutubia wabunge kwa lugha ya Kiingereza na Kijerumani , Merkel amesema kuwa Umoja wa Ulaya ulio pamoja unaweza kuwa mfano kwa maeneo mengine duniani. Hili na sio kitu kingine ni lazima liwe lengo letu. Ameongeza kuwa , ili kuweza kuendeleza lengo hilo tunahitaji Uingereza iliyo imara ikiwa na sauti kubwa ndani ya Umoja wa ulaya . Iwapo tutalifikia hilo tutaweza kufanya mageuzi muhimu kwa ajili ya faida ya kila mmoja wetu.

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari pamoja na kansela Angela Merkel, waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema kuwa nchi hizo mbili zinataka kuimarisha nyanja za ushirikiano. Katika majadiliano yao juu ya mageuzi katika Umoja wa Ulaya Cameron amesema majadiliano hayo yanahitaji kuwahusisha viongozi wengine wa Umoja huo.

Ukraine Kiew Blumen für gefallene Aktivisten auf dem Maidan
Maua kuwakumbuka waliofariki kutokana na maandamano mjini KievPicha: DW/L. Rzheutska

Hatimaye amesema kuwa wamezungumzia kuhusu suala la hali nchini Ukraine na wote wanaunga mkono Ukraine iliyoungana na kutoa onyo kwa Urusi kutoingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo na kuwaachia watu wa Ukraine kuchagua baina ya Urusi na Umoja wa Ulaya.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / rtre

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman