1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel asikitishwa na viwanda vya magari

Sekione Kitojo
21 Agosti 2017

Kansela Angela Merkel alijibu maswali ya wapiga kura katika kipindi cha maswali na majibu cha televisheni, ambapo aliulizwa kuhusu usalama, wahamiaji na kashfa ya kupima moshi unaochafua mazingira kwa magari ya VW

https://p.dw.com/p/2iaMS
Deutschland Merkel Statement zum Barcelona Anschlag
Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Ujerumani mwezi ujao inaendelea.  Bibi Markel Anagombea  muhula  wa  nne. 

Kansela  Angela  Merkel  alishiriki  katika  kipindi  cha televisheni cha  kituo  cha  RTL ambacho  kilikuwa  kinarushwa  moja  kwa moja, Jumamosi  jioni. Wapiga  kura  walimuuliza  maswali  kansela wakati  akiwania  muhula  wa  nne  madarakani  katika  uchaguzi  wa mwezi  Septemba.

USA - Merkel als Malerei: The Art of Leadership in Dallas
Picha ya kuchora ya kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: picture-alliance/dpa/L. W. Smith

Uchunguzi  wa  maoni  ya  wapiga  kura  unaonesha  chama  cha kansela  Merkel  cha  Christian Democratic  Unioni  CDU  pamoja  na chama  ndugu  cha  jimbo  la  Bavaria  Christian Social  Union , CSU vitakuwa  kundi  kubwa  la  chama  bungeni  lakini  bila  ya  wingi  wa kutosha. Kutokana  na  mashambulizi nchini  Ujerumani  na  hivi karibuni  kabisa  mjini  Barcelona, Merkel  aliulizwa  hatua  gani serikali  yake  itachukua  kuimarisha  usalama.

Merkel  alisema  kwamba  mchanganyiko  wa  matumizi  ya  polisi  na matumizi  ya  teknolojia  inapaswa  kutumiwa  kuhakikisha  usalama. Amesema  kwamba  wakati  kuna  raia  wanaokadiriwa  kufikia 10,000   ambao  wamepata  itikadi  kali  na  kuwa  na  mawazo  ya itikadi  kali  nchini  Ujerumani, ni  watu 600  hadi  700  tu wanaonekana  kuwa  ni  hatari.

Merkel  amekosoa  matumizi  ya  Uturuki  ya  jeshi  la  polisi  wa kimataifa  Interpol kumkamata  kwa  kutoa  waranti  na  kutaka arejeshwe  nchini  humo mwandishi Mjerumani  Dogan Akhanli kutoka  nchini  Uhispania  siku  ya  Jumatatu  kuwa  na matumizi mabaya  ya  shirika  hilo  la  polisi  la  kimataifa. "Sio sahihi  na nafurahi  sana  kwamba  uhispania  imemuachia  huru," Merkel amesema. "Hatupaswi  kutumia  vibaya  mashirika  ya  kimataifa kama  Interpol kwa  madhumini  hayo."

Deutschland Bundeskanzlerin Angela Merkel im ARD-Interview
Kansela Angela Merkel akifanyiwa mahojiano na waandishi habari Picha: picture-alliance/dpa/R. Jensen

Kansela achukizwa na  viwanda vya magari

Kansela  amesema  atajaribu  kuunganisha  vifaa  vya  polisi  na utaratibu  wa  majimbo  16  nchini  Ujerumani. Amedokeza  kwamba wengi  hawafahamu upekuzi  wa  polisi  pamoja  na  uangalizi  wa vidio kwamba  unafanyakazi  kwa  njia  tofauti  katika  majimbo  hayo nchini  Ujerumani.

Amesema  chama  chake  cha  Christian Democratic , kitajaribu kuunganisha  mbinu  za  polisi , akisema : "Pia  nitazungumza tena na  mawaziri  wakuu  wa  majimbo  binafsi."

Merkel  pia  alitetea  uamuzi  wake  wa  kufungua  mipaka  ya Ujerumani  kwa  mamia  kwa  maelfu ya  wakimbizi miaka  miwili iliyopita. Alipoulizwa  iwapo  sasa  angefanya  tofauti , alisema: "Bado  nafikiri uamuzi  wangu  ulikuwa  sahihi." Ametoa  wito  wa umoja  zaidi  katika  bara  la  Ulaya  kusaidia  nchi  kama  Italia  na Ugiriki  kupambana  na  idadi  kubwa  ya  wahamiaji  wanaowasili katika  mipaka  yao.

Merkel bei CDA Veranstaltung in Dortmund
Bibi Angela MerkelPicha: picture-alliance/dpa/I.Fassbender

Mpiga  kura  mmoja  aliuliza  swali  kwamba  kwanini  waombaji hifadhi  hawaruhusiwi  kufanyakazi  wakati  kesi  zao  zikifanyiwa mapitio  wakati  baadhi  wakisema  wamesubiri kwa  miaka  kadhaa wakipiewa  fedha  za  walipa  kodi wakati  wanataka  kufanyakazi.

Merkel  amewaambia  wapiga  kura  kwamba  amevunjwa  moyo  na tasnia  ya  makampuni  ya  kutengeneza  magari  kufuatia  kashfa  ya dizeli  ya  kampuni  ya  Vilkswagen. Amesema  waziri  wa  zamani wa  mazingira  alifahamu  madhara  yake. "Nimekasirishwa," Merkel amewaambia  watazamaji. Tasnia  ya  magari  imetishia  kujiingiza katika  matatizo  makubwa   katika  kashfa  hiyo na  makampuni yanapaswa  kujisahihisha  kwa  kiasi  kikubwa kadri wanavyoweza," amedokeza. Amesema  program mpya ipo  kwa  sasa  kuweza kusahihisha  makosa  hayo.

Mwandishi : Jane Mcintosh / ZR / Sekione  Kitojo

Mhariri: Mohammed Abrul Rahman