1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel asisitiza suluhisho la kidiplomasia Ukraine

10 Februari 2015

Rais Barack Obama na kansela wa Ujerumani Angela Merkel jana(09.02.2015) wameelezea juhudi za pamoja za kufikiwa suluhisho la muda mrefu la kidiplomasia katika mzozo kati ya Urusi na Ukraine.

https://p.dw.com/p/1EYxJ
Merkel bei Obama 09.02.2015
Merkel (kushoto) katika mazungumzo na rais Barack Obama (kulia)Picha: S. Loeb/AFP/K. Lamarque

Rais Barack Obama na kansela wa Ujerumani Angela Merkel jana katika Viongozi hao hata hivyo hawajatoa njia ya wazi ya vipi mataifa ya magharibi yataweza kusonga mbele iwapo mazungumzo ya kuleta amani wiki hii yatakwama.

Merkel bei Obama 09.02.2015
kansela Merkel(shoto) na rais Barack Obama(kulia9katika mkutano na waandishi habariPicha: picture-alliance/dpa

Obama ameonesha uwezekano kwamba Marekani inaweza kwa mara ya kwanza kutuma silaha za kupambana na vifaru pamoja na silaha nyingine za kujihami nchini Ukraine. Wakati hakuna uamuzi ambao umekwisha chukuliwa, rais Obama amesema ameamuru kikosi chake kutafakari "Iwapo kuna vitu vingine vya ziada vinavyoweza kufanywa kuisaidia Ukraine kuimarisha ulinzi wake katika mapambano dhidi ya uvamizi wa Urusi.

"Kile nilichokiagiza kikosi changu ni kuangalia hatua mbali mbali za kuchukua. Ni njia gani nyingine zinaweza kuchukuliwa kumfanya Bwana Putin abadilike na uwezekano wa silaha kali za ulinzi ni moja katika nafasi hizo ambazo zinachunguzwa."

Suluhisho la kijeshi

Lakini kansela wa Ujerumani Angela Merkel anapinga vikali kulipatia silaha jeshi la Ukraine lililozingirwa. Kansela wa Ujerumani , ambaye huenda ana uhusiano mzuri zaidi na rais wa Urusi Vladimir Putin , ameweka wazi kwamba hajakata tamaa juu ya uwezekano wa majadiliano ya kidiplomasia kuweza kuleta mpango wa amani ambao hadi sasa haujapatikana.

Staatsbesuch Stephen Harper in Berlin
Kansela Merkel(kulia) katika mkutano na waandishi habari na waziri mkuu wa Canada Stephen HarperPicha: Reuters

"Kila mara imethibitika kuwa ni sahihi kujaribu tena na tena kutatua mzozo kama huu," Merkel amesema.

"Sioni kabisa uwezekano wa suluhisho la kijeshi, lakini tunapaswa kufanyakazi kutafuta zaidi suluhisho la kidiploamsia."

Baadaye jana katika mkutano na waandishi habari pamoja na waziri mkuu wa Canada Stephen Harper, Merkel amesisitiza , "Nina matumaini kwamba tutaweza kutatua mzozo huu kwa njia za kidiplomasia kwasababu nafikiri kwa njia za kijeshi mzozo huu hauwezi kutatuliwa."

Symbolbild Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: SERGEI CHIRIKOV/AFP/Getty Images

Putin anaendeleza sera za kimabavu

Harper amesema anafurahia juhudi za Ujerumani na Ufaransa kuleta suluhisho la amani lakini ameongeza: " Kwa bahati mbaya katika wakati huu Bwana Putin amekataa njia za kidiploamasia. Anaonekana kuelekeza ajenda zake kupitia matumizi ya nguvu.

Wakati huo huo zaidi ya wanajeshi 600 wa Urusi wameanza luteka ya kijeshi katika jimbo la Crimea, leo siku moja kabla ya mkutano kuhusu mzozo wa Ukraine katika mji mkuu wa Belarus Minsk.

Ukraine Soldaten Raketenwerfer Raketen auf Donezk
Mapambano mashariki mwa UkrainePicha: Reuters/Alexei Chernyshev

Nayo majeshi ya serikali ya Ukraine yanaripotiwa kupata mafanikio katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi mashariki mwa Ukraine.

Msemaji wa jeshi la Ukraine Eduard Basurin amesema jana(09.02.2015) kuwa wameuzingira mji wa Debaltseve , ambao umekuwa ukikabiliwa na mapigano makali katika muda wa wiki zilizopita, na kuutenga mji huo na barabara kuu.

Mwandishi: Sekione Kitojo / ape / rtre

Mhariri: Yusuf Saumu