1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel atembelea mataifa ya Balkan

Admin.WagnerD8 Julai 2015

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameanza ziara ya siku mbili kuzitembelea nchi tatu za Balkan ambazo utashi wao wa kujiunga na Umoja wa Ulaya umekuwa ukikwamishwa kutokana na mzozo wa Ugiriki na uhasimu miongoni mwao.

https://p.dw.com/p/1FvFV
Angela Merkel Augen geschlossen
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.Picha: picture-alliance/dpa/Julian Stratenschulte

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewasili katika mji mkuu wa Albania Tirana alikoanzia ziara yake ya siku mbili ya mataifa matatu ya Balkan yanayoomba kujiunga na Umoja wa Ulaya, lakini yalio na safari ndefu kupatiwa uanachama wa jumuiya hiyo.

Mjini Tirana, Merkel amepangiwa kukutana na waziri mkuu Edi Rama na rais Bujar Nishani kabla ya kulihutubia kongamano la wafanyabiashara wa Ujerumani na Albania.

Albania ambayo iliwahi kuwa ngome ya utawala wa kikomunisti wenye msimamo mkali, ilijiunga na jumuiya ya kujihami NATO mwaka 2009 na imetambuliwa kama mgombea wa uanachama wa Umoja wa Ulaya mwaka uliyopita, baada ya ucheleweshaji uliyosababishwa na wasiwasi kuhusu uhalifu wa kupanga na rushwa.

Ziara ya Merkel nchini Albania itakuwa ni ya pili kwa Kansela wa Ujerumani kwa moja ya nchi maskini barani Ulaya tangu mwaka 1999.Maafisa wa Albania waliviambia vyombo vya habari juu ya matakwa yao ya kuzindua mazungumzo kamili ya uanachama haraka iwezekanavyo.

Neuer Präsident Albaniens
Rais wa Albania Bujar NishaniPicha: dapd

Nchi zote hizo zimetangaza matakwa yao ya kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya lakini kutokana na mzozo wa kuiokowa Ugiriki isifilisike na madeni yumkini Merkel na viongozi wengine wa Umoja wa Ulaya wakaweka masharti magumu kwa nchi zinazotaka kujiunga na umoja huo ambazo uchumi wake ni dhaifu.

Serbia na Bosnia walipigana vita katika miaka ya 1990 na kupelekea watu wapato 100,000 kuuawa na mamilioni kuachwa bila ya makazi.Uhusiano wao bado ni wa mvutano na wanaendelea kubishana juu ya kuyaita mauaji ya waislam 8,000 yaliyofanywa na wanajeshi wa Serbia mwaka 1995 kuwa ya kimbari au halaiki, mauaji ambayo yalipekea kuuwa watu wazima na vijana. Hadi sasa mahakam mbili za umoja wa mataifa zinayaita mauaji hayo ni ya kimbari.

Serbia inakataa kuutambua uhuru wa Jimbo lake la zamani la Kosovo, jambo ambalo linaungwa mkono na Albania, kitendo ambacho uwenda kikaiondoa ndoto ya Serbia kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Nchi hiyo imegaika kati ya wale wanaopendelea kujiunga na Umoja wa Ulaya na wale wanaopendelea kuwa karibu zaidi na Urusi-mshirika wa jadi wa waserbia.Kansela Angela Merkel atakutana na wote wawili;waziri mkuu anaelemea upande wa umoja a Ulaya Aleksander Vuvic na rais anaelemea upande wa Urusi Tomislav Nikolic.

Anataraajiwa kuwaeleza kwamba Serbia haitoweza kujiunga na Umoja wa Ulaya kabla ya kwanza kuwa na uhusiano wa ujiraani mwema pamoja na Kosovo na Bosnia.Jambo hilo waserbia daaima wamekuwa wakiliangalia mwanzo wa kutambuliwa rasmi taifa la Kosovo na kuwaachilia mbali ndugu zao wa kiserbia nchini Bosnia.

Maafisa wa Kosovo na Serbia wamekuwa wakiendeleza mazungumzo chini ya upatanishi wa Umoja wa Ulaya kuhusu mustakbal wa uhusiaano wao wa siku za mbele-lakini matokeo ya mazungumzo hao mpaka sasa ni finyu.

Nchini Bosnia Merkel atawahimza kuanzisha shuguli ya kijamii na kiuchumi ambazo zitaleta mageuzi ya kutengeza ajira na kuileta nchi karibu na uanachama wa Umoja wa Ulaya.

Mwandishi:Salma Mkalibala/DPA,APE

Mhariri: Iddi Ssessanga