1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel -Kaukasus

26 Agosti 2008

Kanzela Merkel wa Ujerumani anazuru Estonia na baadae Lithunia kuhusu mzozo wa Georgia..

https://p.dw.com/p/F59g
Merkel akiwa TalinnPicha: picture-alliance/ dpa

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani alikutana leo na waziri mkuu wa Estonia, Andrus Ansip kwa mazungumzo juu ya mgogoro wa Kaukasus.Katika ziara yake hii ya Estonia na Lithuania,Kanzela Merkel anazungumzia msimamo wa Umoja wa Ulaya kuelekea Russia kutokana na mzozo wa Russia na Georgia.Nchi za bahari ya baltik zinadai kuchukuliwa msimamo mkali dhidi ya Russia.

►◄

Kanzela Angela anahimiza kuwa majeshi ya russia yaondolewe kutoka Gorgia kulingana na mpango wa amani wa mambo 6 ulioafikiwa na Russia.Pia anapendekeza mazungumzo na Moscow.Mada nyengine katika mazungumzo yake na waziri mkuu wa Estonia ni lile bomba la kusafirishia gesi kutoka Russia hadi Ujerumani.

Kanzela Merkel anatarajia nchi zanachama wa Umoja wa Ulaya zitakuwa na msimamo mmoja kuelekea Russias .Anasisitiza kwamba kuheshimiwa kwa mamlaka ya ardhi ya georgia ni sharti la ushirikiano wa kimataifa na Russia.

Amedai wakati huo huo mlango ubakie wazi kwa mazungumzo na Russia.Mwenyeji wake waziri mkuu wa estonia, mjini Talinn amedai mazungumzo hayo yasifanyike kabla ya Russia kutekeleza masharti ya huo mpango wa amani wa mambo 6.

Baadae Kanzela Merkel alihutubia wajumbe wa kisiasa,kiuchumi na wataalamu wa kisayansi katika Makumbusho ya sanaa.

Kabla hakuelekea nchi jirani ya Lithuania, Kanzela Merkel alikuwa na mazungumzo na rais Toomas Ilves wa Estonia.Ilves wiki mbili tu nyuma aliweka shaka shaka zake juu ya ushirika wa kimkakati baina ya umoja wa ulaya na Russia.

Kanzela Merkel wa Ujerumani alianza ziara yake hii ya siku 2 hapo jana mjini Stockholm,Sweden.Baada ya mazungumzo yake na waziri mkuu wa sweden Frederik Reinfeldt alilieleza lile azimio lililopitishwa jana na Bunge la Russia kuutambua eneo la kusini mwas Ossetien na Abchasia kuwa ni nchi huru zilizojitenga na Georgia.

Akisisitiza kwamba suluhisho laweza tu kupatikana kupitia mazungumzo,Kanzela wa Ujerumani, anapanga kukutana na rais wa russia kwa mara nyengine tena hapo Oktoba 2.Wakati huo kitafanyika kile kikao cha ushauriano baina ya ujerumani na Russia,mjini St.Petersburg.