1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel kukutana na Hollande

22 Septemba 2012

Viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wanakutana Jumamosi(22.09.2012)kuadhimisha hotuba iliyotolewa1962 na Charles de Gaulle,huku mzozo wa euro na pendekezo la kuunganisha makampuni ya EADS na BAE yakiwa katika agenda.

https://p.dw.com/p/16CbG
German Chancellor Angela Merkel welcomes French President Francois Hollande at the Chancellery in Berlin, May 15, 2012. Hollande called for a European pact for growth to balance out German-driven austerity measures in his inaugural address on Tuesday, hours before taking his challenge to Chancellor Angela Merkel in Berlin. Sworn in with all the pomp of the French Republic, Hollande won support from Germany's opposition Social Democrats (SPD), who vowed to use their parliamentary blocking power to delay ratifying a European budget discipline treaty until Merkel accepts accompanying measures to boost growth and jobs. REUTERS/Fabrizio Bensch (GERMANY - Tags: POLITICS)
Merkel na Hollande wakutanaPicha: Reuters

Msemaji wa kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa mkutano huo utakaofanyika katika mji wa Ludwigsburg kusini magharibi mwa Ujerumani , ambako De Gaulle alitoa hotuba hiyo kwa vijana wa Ujerumani katika hatua muhimu ya maridhiano baada ya vita vikuu vya pili vya dunia, utakuwa tu kwa kiasi kikubwa kwa ajili tu ya heshima za sherehe za maadhimisho.

Lakini mada chache muhimu hata hivyo zitakuwa katika agenda ya majadiliano.

Suala la kampuni la kuunda vyombo vya usafiri wa anga la EADS na lile la Uingereza la BAE bila shaka litazungumzwa katika chakula cha mchana kitakachotumiwa kufanya majadiliano hayo pamoja na rais Francois Hollande, msemaji huyo , Steffen Seibert, amewaambia waandishi habari Ijumaa, (21.09.2012), akilenga kuhusu mkutano huo ambao haukutangazwa sana.

HANDOUT - Ein Schiff steht hinter dem Schriftzug von BAE Systems in Henderson, WA (undatiertes Handout). Der britische Rüstungskonzern BAE Systems hat Fusionsgespräche mit dem größten europäischen Luft- und Raumfahrtkonzern EADS bestätigt. Sollte es zu einer Fusion kommen, würde EADS den US-amerikanischen Rivalen Boeing beim Umsatz nicht nur überholen, sondern sogar deutlich abhängen. Foto: BAE Systems
Kampuni ya Uingereza ya BAE inazungumza na EADS kutana kuunganaPicha: picture-alliance/dpa

"Bila shaka hakutakuwa na maamuzi Jumamosi hii na msiende katika mkutano huo wa waandishi habari mkitarajia kutakuwa na jambo lolote la maamuzi," alisema Seibert. Hii pia itakuwa pamoja na suala la udhibiti mkali wa sekta ya benki katika bara la Ulaya , mtazamo wa mapambano dhidi ya mzozo wa madeni katika eneo la euro kwa wakati huu, Seibert amesema.

Serikali zimekuwa zikichukua tahadhari tangu kutangazwa wiki iliyopita kuwa kampuni ya vifaa vya ulinzi nchini Uingereza BAE na kampuni linayotengeneza ndege katika bara la Ulaya EADS yanafanya majadiliano ya kuungana.

Rais wa Ufaransa amesema kuwa Paris na Berlin zinasubiri mradi huo wa kuungana kufafanuliwa kabla ya kupitisha maamuzi na kuchukua uamuzi.

Ujerumani pia imechukua msimamo wa kusubiri na kuona, huku baadhi ya maafisa wakitia shaka kuwa muungano huo unaweza kusababisha ukosefu wa ajira.

Hamburg/ Mitarbeiter montieren am Dienstag (17.01.12) in Hamburg in einer Werkhalle des Luftfahrtkonzerns Airbus Flugzeuge der Airbus A320-Familie. Viele Flugzeuge verkauft, aber wenig Gewinn gemacht - das soll fuer den europaeischen Luft- und Raumfahrtkonzern EADS und die wichtigste Tochter Airbus endlich Vergangenheit sein. "EADS ist eine Cash- und Wachstumsmaschine. Jetzt ist es an der Zeit, die Rentabilitaet zu steigern", sagte der Vorstandsvorsitzende Louis Gallois am Dienstag auf der Jahrespressekonferenz in Hamburg. Airbus verzeichnete im vergangenen Jahr mit 1.608 Neubestellungen das beste Jahr seiner Geschichte und verwies den ewigen Konkurrenten Boeing mit 921 Bestellungen auf den zweiten Platz.
Kampuni inayounganisha ndege za Airbus EADS A320Picha: dapd

Makampuni hayo mawili yamepewa hadi Oktoba 10 kukamilisha mradi wao ama waachane nao. Ujerumani na Ufaransa zina hisa nyingi katika kampuni la EADS, wakati serikali ya Uingereza ina hisa kubwa katika kampuni la BAE ambazo zinairuhusu kutumia kura ya turufu kuzuwia maamuzi ambayo inayaona kuwa hayaendani na maslahi ya umma.

Wakati Ufaransa inapendelea kutoa madaraka kwa benki kuu ya Ulaya kuangalia benki zote 6,000 za eneo la mataifa ya euro kuanzia mwezi Januari, Ujerumani inataka kuziangalia benki kubwa tu na haiko katika hali ya kuharakisha, ikipendelea udhibiti wa kina kwanza badala ya haraka.

Sherehe za Jumamosi ni za hivi karibuni kabisa katika wimbi la matukio ya maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano kati ya mahasimu hao wa wakati wa vita.

Merkel na Hollande watakutana katika kasri la Baroque mjini Ludwigsburg, watatoa maelezo kidogo na kisha watarejea katika shughuli za majadiliano pamoja na kupata chakula cha mchana. Viongozi hao , ambao wanajaribu kuweka msuguano wao katika kiwango cha chini tangu rais Hollande kuingia madarakani mwezi Mei, wanatarajia kuwa na mkutano wa pamoja na waandishi habari mchana.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe

Mhariri : Iddi Ismail Ssessanga