1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Messi na baba yake watuhumiwa kukwepa kodi

12 Juni 2013

Waendesha mashtaka wa serikali kuhusu masuala ya fedha wamefungua malalamiko wakimtuhumu mchezaji maarufu wa soka wa klabu ya Barcelona Leonel Messi kwa ugandanyifu wa kulipa kodi unaokadiriwa kufikia euro milioni tano.

https://p.dw.com/p/18oVk
Barcelona's Argentinian forward Lionel Messi gestures during UEFA Champions League semi final first leg football match between FC Bayern Munich and FC Barcelona on April 23, 2013 in Munich, southern Germany. AFP PHOTO / PIERRE-PHILIPPE MARCOU (Photo credit should read PIERRE-PHILIPPE MARCOU/AFP/Getty Images)
Mchezaji wa Barcelona Lionel MessiPicha: PIERRE-PHILIPPE MARCOU/AFP/Getty Images

Duru za mahakama zimesema leo kuwa malalamiko hayo , ambayo pia yanamjumuisha baba wa mchezaji huyo Horacio Messi kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uhispania , yamewasilishwa mahakamani.

Duru hizo zimesisisitiza hata hivyo kuwa haifahamiki bado iwapo mahakama itayakubali malalamiko hayo na kuruhusu mashtaka kuendelea.

Klabu ya Barcelona haikuweza kutoa maelezo yake mara moja.

Togo wagoma

Wachezaji kandanda wa timu ya taifa ya Togo wanakataa kucheza mchezo wa kutafuta kufuzu katika fainali za kombe la dunia nchini Libya baada ya ghasia za hivi karibuni nchini humo na kusababisha shirikisho la kandanda la dunia , FIFA kuuhamisha mchezo huo uliopangwa kuchezwa siku ya Ijumaa kutoka mjini Benghazi hadi katika mji mkuu Tripoli.

Alexis Romao wa klabu ya Marseille na Jonathan Ayite wa klabu ya Brest wamerejea nchini Ufaransa kutoka Togo wakielezea hofu ya usalama kuwa sababu ya hatua yao hiyo ya kutotaka kwenda Libya. Wachezaji wa Togo wanataka mchezo huo uhamishwe kutoka Libya .

Togo's Emmanuel Adebayor (4) celebrates scoring a goal during their African Nations Cup Group D soccer match against Tunisia in Nelspruit, January 30, 2013. REUTERS/Thomas Mukoya (SOUTH AFRICA - Tags: SPORT SOCCER)
Wachezaji wa timu ya TogoPicha: Reuters

Soka ya Togo imekumbwa na maafa kadha hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kuanguka kwa helikopta katika uwanja wa ndege wa Sierra Leone mwaka 2007 na shambulio dhidi ya basi lililokuwa likiwapeleka wachezaji wa timu hiyo kwenda Angola mwaka 2010.

Nahodha wa Togo Serge Akakpo amesema kuwa baada ya kile kilichowatokea huko Lungi na Cabinda, inaeleweka kwa nini wako sahihi kukataa kuhatarisha maisha yao.

Uturuki kuwa mwenyeji wa kombe la dunia

Wakati huo huo rais wa shirikisho la kandanda duniani FIFA Sepp Blatter amesema kuwa fainali za kombe la dunia kwa vijana wa umri wa chini ya miaka 20 zitafanyika wiki ijayo nchini Uturuki licha ya ghasia za kuipinga serikali mjini Stanbul na kwingineko nchini humo.

Fussball 63. FIFA Kongress auf Mauritius 2013 30.05.2013 FIFA Praesident Joseph S. Blatter (Schweiz) eroeffnet den Kongress FOTO: Pressefoto ULMER/Markus Ulmer xxNOxMODELxRELEASExx
Rais wa FIFA Sepp BlatterPicha: picture alliance / Pressefoto ULMER/Markus Ulmer

Fainali hizo zinazohusisha timu za mataifa 20 zimepangwa kufanyika kuanzia Ijumaa wiki ijayo katika miji saba nchini Uturuki, nchi ambayo imeshuhudia wiki mbili za ghasia za kuipinga serikali.

Blatter amesema leo(12.06.2013) kuwa FIFA inafanya mawasiliano na maafisa wa Uturuki, hususan usalama. Ameongeza kuwa garantii zimetolewa na ana hakika kuwa hakuna kitu kitakachotokea.

Mwandishi: Sekione Kitojo

Mhariri: Yusuf saumu