1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Messi na babake watakiwa kufika mahakamani

21 Juni 2013

Jaji nchini Uhispania ameyakubali madai ya kukwepa kulipa kodi yanayomkabili mchezaji bora wa mwaka mara nne Lionel Messi na babake Jorge, na kuanzisha uchunguzi dhidi yao

https://p.dw.com/p/18tm1
Bildnummer: 13789638 Datum: 05.04.2011 Copyright: imago/Marca Barcelona training session, in this picture Lionel Messi and his father Jorge Horacio xFRANCESCxADELANTADOx PUBLICATIONxINxGERxAUTxHUNxONLY ; Fussball ESP Primera Division 2010 privat Familie Vater premiumd x0x xsk 2011 hoch Image number 13789638 date 05 04 2011 Copyright imago Marca Barcelona Training Session in This Picture Lionel Messi and His Father Jorge Horacio PUBLICATIONxINxGERxAUTxHUNxONLY Football ESP Primera Division 2010 Private Family Father premiumd x0x xsk 2011 vertical
Lionel Messi und Vater JorgePicha: imago/Marca

Messi ametakiwa kufika mahakamani Septemba 17. Mahakama moja ya Uhispania katika mji wa Gava karibu na Barcelona jana ilikubali kesi hiyo iliyowasilishwa na mwendesha mashitaka wa umma Raquel Amada wiki iliyopita. Jaji alimtaja Lionel Messi kama mshukiwa katika uchunguzi wa kukwepa kulipa kodi na akamtaka mshambuliaji huyo wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina kufika mahakamani Septemba 17.

Uchunguzi wa kukwepa kulipa kodi

Kikao hicho cha kuskizwa kesi yake mwezi Septemba kitakuwa sehemu ya uchunguzi wa mwanzo kuhusiana na kesi hiyo, ili kubainisha kama kuna ushahidi wa kutosha kumfungulia mashtaka rasmi Messi au babake Jorge Messi kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.

Muargentina Lionel Messi ameimarika na kuwa jina maarufu kote ulimwenguni katika kandanda
Muargentina Lionel Messi ameimarika na kuwa jina maarufu kote ulimwenguni katika kandandaPicha: picture-alliance/dpa

Madai dhidi ya Messi yanahusu mapato ya kodi ya mwaka wa 2007, 2008 na 2009. mwendesha mashitaka Amada alisema mnamo Juni 12 kuwa Messi alikuwa na deni la kodi la kiasi cha euro milioni nne kutokana na malipo aliyopata katika mauzo ya haki za picha yake. Jorge Horacio Messi anahudumu kama mmoja wa mawakala wa mwanawe tangu alipojiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 16 mnamo mwaka wa 2004.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina ameimarika na kuwa jina maarufu kote ulimwenguni katika kandanda, mshindi wa mataji manne mfululizo ya Mchezaji bora wa mwaka wa FIFA na pia mshambuliaji bora zaidi katika historia ya klabu ya Barca.

Pia alikuwa mfungaji wa magoli mengi zaidi katika msimu uliokamilika wa ligi kuu ya soka Uhispania La Liga, kwa kufunga zaidi y agoli moja katika kila mechi na kuisaidia Barcelona kurejesha kabatini taji ambalo walipokonywa awali na Real Madrid mwaka wa 2012.

Mwandishi: Bruce Amani/ (AFP, AP)

Mhariri: Josephat Charo