1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Messi mchezaji bora wa mwaka Ulaya

28 Agosti 2015

Lionel Messi ameshinda tuzo ya UEFA ya mchezaji bora barani Ulaya kwa mara ya tatu, na kumpiku Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na mwenzake wa Barca Luis Suarez.

https://p.dw.com/p/1GNZ7
Monaco Fußballer Lionel Messi UEFA Preis 2015
Picha: picture-alliance/dpa/G. Horcajuelo

Akiwa na magoli 58 katika michuano 57, Messi aliiongoza Barcelona kutwaa mataji matatu msimu uliopita – Champions League, ubingwa wa Uhispania (La liga) na Kombe la Mfalme. Chini ya uongozi wa kocha Luis Enrique, mchezo wa Messi umekuwa wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na lishe bora na kujitolea katika mazoezi.

Katika kiwango cha kimataifa, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alikuwa nguzo muhimu katika matokeo ya Argentina kufikia fainali ya mwaka jana ya Kombe la Dunia ambako walishindwa na UJERUMANI mjini Rio de Janeiro.

Mwaka huu, Messi na Argentina walitinga katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Amerika Kusini – Copa America, lakini timu yake ilishindwa na Chile walioshinda dimba hilo kwa mara ya kwanza.

Mwandishi. Bruce Amani/DW/AFP/DPA/AP/reuters
Mhariri: Mohamed Khelef