1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MEXICO CITY: Maafisa 300 wa polisi wasimamishwa kazi

26 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoH

Mexico imewasimamisha kazi maafisa wa polisi takriban 300 na inawalazimisha wakamilishe mpango dhidi ya ufisadi na rushwa kabla kuruhusiwa warejee kazini.

Waziri wa usalama wa raia, Genaro Garcia Luna, amewaambaia waandishi wa habari mjini Mexico City kwamba mpango huo utajumulisha maafisa hao kupimwa ikiwa walitumia dawa za kuongeza nguvu misuli, na kuulizwa maswali kupima saikolojia yao.

Waziri huyo amesema fedha na mali zinazomilikiwa na maafisa hao wa polisi zitachunguzwa ili kutathmini ikiwa zinaenda sambamba na mishahara yao.

Hatua hiyo ni sehemu ya kampeni ya rais wa Mexcio, Felipe Calderon, dhidi ya biashara haramu za dawa za kulevya.

Maafisa wa polisi nchini Mexico wamekuwa wakishutumiwa kwa ufisadi na ulaji rushwa na kushirikiana na magenge ya wafanyabiashara ya dawa za kulevya.