1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MEXICO CITY: Maelfu ya watu Mexico wangojea misaada

5 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79u

Rais wa Mexico Felipe Calderon ameomba msaada wa jumuiya ya kimataifa kukabiliana na maafa yaliyosababishwa na mafuriko.Asiliamia 80 ya jimbo la Tabasco limefurika na juhudi za kuwaokoa maelfu ya watu waliokwama kwenye mapaa ya nyumba zao Tabasco zinaendelea.Zaidi ya watu milioni moja wamepoteza makaazi yao.Rais Calderon amesema hayo ni maafa mabaya kabisa kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni nchini Mexico.