1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MEXICO CITY: Ziara ya Bush Mexico yakabiliana na maandamano

14 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJC

Rais George W.Bush wa Marekani ameahidi kuchukua hatua za kubadilisha sera za uhamiaji za nchi yake kuhusu raia wa Mexico.Bush alitamka hayo mwanzoni mwa mkutano wake na rais wa Mexico, Felipe Calderon mjini Mexico City.Kwa upande mwingine,Rais wa Mexico aliukosoa mpango wa Marekani wa kutaka kujenga uzio wa maili 700 mpakani.Vile vile ametoa wito kwa Bush kuchukua hatua zaidi kuzuia biashara ya madawa ya kulevya kwenye mpaka wa nchi hizo mbili.Baada ya Rais Bush kuondoka mji mkuu wa Mexico,mamia ya waandamanaji wanaopinga ziara hiyo waliwarushia mawe polisi wa kuzuia ghasia waliokuwa wakilinda ubalozi wa Marekani.Polisi waliwatawanya waandamanaji hao kwa kutumia gesi ya kutoa machozi na watu 3 walikamatwa.