1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Abdulla wa Saudi Arabia ziarani nchini Syria

Jane Nyingi/ AFPE8 Oktoba 2009

Ni ziara ya kihistoria baada ya uhusiano mbaya.

https://p.dw.com/p/K2Mi
Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia na Rais Assad wa Syria mjini Damascus.Picha: AP

Mfalme Abdullah bin Abdulaziz wa Saudi Arabia hii leo Alhamisi, amekamilisha ziara yake ya kihistoria nchini Syria. Wakati wa ziara hiyo ya siku mbili mfalme Abdullah alifanya mazungumzo ya kisiasa na kiuchumi na rais wa Syria Bashar al Assad.

Saudia Arabia imeitaka Syria kushiriki katika juhudi za kutatua matatizo miongoni mwa wapalestina, kuunga mkono Iraq na Lebanon na vilevile kushirikiana kupambana na ugaidi na pia wafuasi wa itikadi kali katika eneo hilo.

Mfalme Abdullah aliwasili nchini Syria jana jumatano, katika ziara ambayo imetajwa kuwa ya kihistoria na mwamko mpya wa uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili. Syria na Saudi Arabia ni mataifa mawili ya kiarabu ambayo yamekuwa na uhasama wa muda mrefu huku Saudi Arabia ikiwa na uhusiano wa karibu na Marekani, na Syria kwa upande ule mwingine ikipinga vikali ushawishi wa Marekani katika eneo hilo.

USA Soldaten üben in Kuwait
Vita vya Irak vilikua chanzo cha uhusiano kuzorota.Picha: AP

Zaidi mzozo kati ya mataifa hayo mawili imechochewa na Syria kuwa na uhusiano wa karibu na Iran. „“Ilikuwa ziara iliyozaa matunda na kufanyika katika mazingira kuelewana .Upande wa Syria na Saudi Arabia umeeleza kuridhishwa na mazungumzo hayo„ amesema mahariri wa gazeti la al -Watan nchini Syria ,bw Abd Rabbo.

Hapo jana rais Assad alimtuza mfalme Abdullah medali ya kitaifa ya Umayya,ambayo ni ya juu zaidi nchini Syria, huku mfalme wa Saudia akimtuza medali ya Ufalme huo rais Assad. Katika muda wa miaka kadhaa iliyopita Syria imekuwa ikijizatiti kuweka kando tofauti kati yake na Saudia na kutafuta msimamo mmoja amesema mwandishi huyo wa habari Abd Rabbo.

Hii ni ziara ya kwanza ya mflame Abdullah nchini Syria tangu alipoingia madarakani mwaka 2005. Marchi iliyopita,Saudia ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele uliofanyika mjini Riyadh kuimarisha uhusiano miongoni mwa mataifa ya kiarabu. Mkutano huo uliwaleta pamoja mfalme Abdullah,rais Assad wa Syria, Hosni Mubarak wa Misri na mfalme Sheikh Sabah al-Ahmad al Sabah wa umoja wa falme za kiarabu.

Rais Assad amesema ziara hiii imeimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya matiafa hayo mawili baada ya miaka mingi ya uhusiano usiokuwa mzuri kutokana na tofauti kuhusiana na Palestina na Iran.Syria inaunga mkono wapiganaji wa kundi la Hamas huku saudia na Misri zinaunga mkono kundi la Fatah linaloongozwa na rais Mohmoud Abbad wa Palestina.

Uhusiano kati ya Syria na Saudia ulizorota baada ya Marekani kuivamia Iraq mwaka 2003,kutokana na Saudi Arabia kuiunga mkono Marekani.

Mwandishi:Jane Nyingi/DPAE

Mhariri:Abdul-Rahman