1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfaransa Mahkamani Chad

23 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CfPR

NAIROBI:

Mfanyakazi wa kifaransa anaekabiliwa na mashtaka pamoja na wenzake 5 kuhusika na ile njama ya kunyakuliwa watoto 100 wa kiafrika nchini Chad ,ameiambia Mahkama kwamba walihadaiwa juu ya utambulisho hasa wa watoto hao.

Emilie Lelouch, mwanachama wa shirika la misaada la kifaransa (Zoe’s Ark) ameiambia Mahkama kuwa kundi lao lilihadaiwa juu ya watoto hao na walkiamkni kwa dhati wote ni mayatima kutoka mkoa wa Dafur,Sudan .

Uchunguzi uliofanywa pale watumishi wa misaada walipokamatwa Oktoba mwaka huu ulibainisha wengi wa watoto hao 103 wakiishi alao na mzazi wao mmoja au jamaa zao na hawakutoka mkoa huo wa Sudan,wenye msukosuko.

Kesi hii ilifunguliwa ijumaa iliopita na raia hao 5 wa kifaransa wanaohukumiwa pamoja na wachadi na msudani waweza kuhukumiwa hadi miaka 20 korokoroni.