1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfungamano wa serikali ya mseto kushughulikiwa zaidi

22 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQQ3

Naibu mpya wa Kansela wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amesema,katika majuma yajayo atashughulikia kuleta mfungamano zaidi katika serikali ya mseto.Akisisitiza wajibu wa serikali ya mseto kwa Ujerumani na Ulaya,Steinmeier amesema,serikali hiyo ya mseto haiwezi kumudu kufanya kampeni za uchaguzi kwa miaka miwili ijayo.

Steinmeier alipokea wadhifa wake mpya siku ya Jumatano,baada ya Franz Münterfering aliekuwa waziri wa ajira,kujiuzulu kama naibu Kansela.Olaf Scholz aliekuwa kiongozi wa SPD bungeni,sasa ni waziri mpya wa ajira.