1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgogoro wa Kirgistan,138 wafa

Abdu Said Mtullya15 Juni 2010

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lalaani matukio ya umwagaji damu nchini Kirgistan.

https://p.dw.com/p/NqqT
Mtu wa jumuiya ya wakirgiz akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa katika ghasia zinazoendelea nchini Kirgistan.Picha: AP

NEW YORK:

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mapambano yanayosababisha damu kumwagika nchini Kirgistan.

Baraza hilo limetoa mwito wa kuumaliza mgogoro ulioikumba nchi hiyo unaotokana na mvutano baina ya watu wa jamii za wakirgiz na wauzbeki.Kwa niaba ya Baraza hilo balozi wa Mexico Claude Heller ametoa mwito wa misaada kwa watu wa Kirgistan.

Tokea ghasia zianze nchini humo wiki iliyopita kutokana na mvutano baina ya Wakirgiz na Wauzbek,ambao ni jamii ya wachache, watu zaidi ya 130 wameshakufa na wengine 1800 wamejeruhiwa.Maalfu wengine wamekimbilia katika nchi jirani ya Uzbekistan.

Ili kukabiliana na matukio ya nchini Kirgistan Urusi kwa kushirikiana na nchi za mfungamano wa ulinzi wa nchi zilizokuwa chini ya himaya ya kisoviet zinafikiria kupeleka ndege aina ya helikopta na magari.

Katibu Mkuu wa mfungamano huo OVKS, Nikolai Bordyusha amesema Kirgistan ina majeshi ya kutosha lakini inahitaji zana zaidi za kijeshi.