1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Usalama mjini Munich

15 Februari 2016

Kansela Angela Merkel na kishindo cha wakimbizi,mkutano wa usalama mjini Munich na vuta nikuvute kuhusu jaji wa korti kuu ya Marekani ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa zaidi na wahariri wa magazeti ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/1HvWN
Wajumbe katika mkutano wa Usalama mjini MunichPicha: Reuters/M. Dalder

Tuanzie lakini na kishindo cha wakimbizi.Magazeti mengi yanahisi kansela yuko katika hali ya upweke na sera zake za ukarimu kuelekea wakimbizi. Gazeti la "Landeszeitung" limeandika:"Mpaka katika siasa ya nje na hasa wakati huu wa kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya,kansela Angela Merkel anajikuta ametengwa zaidi kuliko wakati wowote ule mwengine. Mzozo wa wakimbizi ni kizungumkuti kikubwa kwa Umoja wa ulaya.Mpaka nguzo ya Ujerumani na Ufaransa inaonyesha si madhubuti sana. Manuel Valls ameyavunja matumaini ya kansela ya mshikamano imara katika kugawana mzigo wa wakimbizi barani Ulaya kwamba kundi la nchi nne za Ulaya ya kati mashariki zinaupinga mkakati wa kansela,na kwamba Macedonia inataka kujenga ukuta wa kinga,yote hayo yalikuwa yakitarajiwa. Lakini La bayana ya Ufaransa haikutolewa wakati muwafak. Na kama hilo ndilo jibu kwa Ujerumani iliyoonyesha mshikamano na Ufaransa na kufika hadi ya kujiunga katika opereshini za kijeshi nchini Syria,basi mtu anaweza kusema mustakbal wa ulaya hauashirii mema.

Kitisho cha kutokea vita vyengine vikuu

Mzozo wa Syria umegubika mkutano wa Usalama mjini Munich. Gazeti la "Thüringische Landeszeting" limeandika: "Kimsingi watu hawawezi kufanya chochote si pamoja na wala si bila ya Urusi. Kwa sababu kwa upande mmoja makubaliano kuhusu Syria hayajadumu hata saa 48 ,mwakilishi wa Urusi ameshayavuruga. Hakuna anaeyaamini makubaliano ya kuwewka chini silaha,na Marekani nayo puia haitaki ushirikiano wa dhati. Kwa aupande mwengine hakuna kinachowezekana bila ya Urusi-bila ya nchi hiyo,watu hawawezi kuamua kuhusu mustakbal wa Syria na eneo hilo kwa jumla. Dhahir hapo ni kwamba Urusi inatumia ushawishi wake kupigania kwanza masilahi yake. Kuhakikisha usalama ni suala linalokamata nafasi ya pili.

Kinyang'anyiro cha kuania madaraka Marekani

Kifo cha ghafla cha jaji Antonin Scala wa korti kuu ya Marekani kimesababisha mvutano warepublican wakidai jaji mpya anabidi achagzuliwe na rais atakaechaguliwa baada ya uichaguzi wa novemba nane huku wademocrates na rais Barack Obama wakihoji kinyume chake. Gazeti la "Emder-Zeitung" limeandika kuhusu kasheshe hiyo:"Scalia alikuwa mwanasheria wa kihafidhina.Alikuwa akiunga mkono adhabau ya kifo,akipinga watu kuharibu mimba,akipigania mshikamano wa dhati kati ya shughuli za serikali na za kidini,haki ya kumili na kubeba silaha na kadhalika. Sasa mvutano umeripuka kuhusu nani wa kushika nafasi yake. Rais Obama angependelea kumteuwa mwanasheria mwenye msimamo wa wastani-warepublican wanapinga.Wanadai rais mpya ndie anaestahiki kumteuwa jaji atakaeshika nafasi ya Scala. Kwa hivyo kiti chake kitakuwa kitupu kwa mwaka mzima. Mfumo huru wa sheria una sura nyengine kabisa. Kifo cha jaji wa korti kuu na nani wa kushika nafasi yake limegeuka kinyang'anyiro cha kuania madaraka. Kinyang'anyiro kati ya Republikan kwa upande mmpoja na Democrats na rais Obama kwa upande wa pili.Kwasababu ya wadhifa wa jaji-ni shida kulielewa hilo.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman