1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgombea wa upinzani apigwa risasi kabla ya uchaguzi

22 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CRu5

Siku 10 kabla ya kufanywa uchaguzi wa bunge nchini Urusi,mgombea wa upinzani amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana.Farid Babayev wa chama cha wastani cha Yabloko Party alipigwa risasi mbele ya nyumba yake Jumatano usiku katika mji mkuu wa Jamhuri ya Dagestan,Makhachkala.

Rais Vladimir Putin wa Urusi siku ya Jumatano katika mkutano wa kampeni mjini Moscow, aliwatuhumu vikali wanasiasa wa upinzani kuwa wanadhaminiwa na nchi za kigeni.Putin ni mgombea mkuu wa chama cha Muungano wa Urusi katika uchaguzi utakaofanywa tarehe 2 Desemba.Iwapo chama chake kitashinda,basi Putin ataweza kushika wadhifa wa waziri mkuu.Awamu yake kama rais wa Urusi inamalizika mapema mwaka ujao.