1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo wa Benki ya NMB nchini Tanzania

24 Septemba 2008

Nchini Tanzania, mahakama kuu ya nchi hiyo kitengo cha kazi jana ilitoa amri ya kuwataka wafanyakazi wa benki kubwa kabisa nchini humo ya NMB kubatilisha mgomo wao uliyoanza Jumatatu.

https://p.dw.com/p/FOHs

Wafanyakazi hao waliitisha mgomo huo kama njia ya kushinikiza kutekelezwa kwa matakwa yao ambayo ni kusainiwa kwa makubaliano ya kulipwa asilimia tano ya hisa pamoja na fedha za mfuko wa kujikopesha. Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo Ernest Mwaipopo aliwataka wafanyakazi hao kurejea kazini kuanzia saa mbili asubuhi leo hii.

Ili kufahamu ni vipi amri hiyo imetekelezwa Aboubakary Liongo alizungumza na mwenyekiti wa kamati ya wafanyakazi hao, Joseph Masana.