1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo wa magari ya abiria ya Matatu nchini Kenya

8 Aprili 2009

Nchini Kenya mgomo wa magari madogo ya abiria maarufu matatu umeingia siku yake ya pili katika mji wa Nairobi.

https://p.dw.com/p/HSw4
Jiji la Nairobi lakabiliwa na mgomo wa usafiri wa MatatuPicha: DW

Kulingana na wahudumu wa matatu malalamiko yao yanajumuisha kuhangaishwa na maafisa wa polisi wakati wanapoendesha shughuli zao pamoja na ada wanazolazimika kuwalipa wafuasi wa Mungiki wanaosimamia baadhi ya vituo.Kutokana na mgomo huo mamia ya wakazi wa jiji la Nairobi walilazimika kutembea mwendo mrefu ndipo waweze kufika katika sehemu zao za kazi.

Mwandishi wetu wa Nairobi Eric Ponda ametuandalia taarifa ifuatayo.

Mwandishi: Eric Ponda
Mhariri: Mohamed Abdulrahman