1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo wa wafanyakazi wa shirika la reli waendelea.

21 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQ2S

Paris. Vyama vya wafanyakazi wa usafirishaji nchini Ufaransa , utawala na serikali wanatarajiwa kuwa na mazungumzo wakati mgomo dhidi ya mipango ya mageuzi ya akiba ya uzeeni yakiingia katika siku yake ya nane. Matumaini yameongezeka kuwa makubaliano yanaweza kufikiwa na kumaliza mgomo huo ambao umedhoofisha mfumo mzima wa usafirishaji nchini Ufaransa. Mamia kwa maelfu ya wafanyakazi wa umma waliongeza mbinyo wao katika mgomo huo jana Jumanne kuhusiana na wasi wasi wao wa kupoteza kazi. Rais Nocolas Sarkozy ameahidi kuendelea na mageuzi yake yanayoonekana kupingana na matarajio ya watu wengi. Shirika la taifa la reli, SNCF, limekadiria kuwa kutakuwa na hali bora ya huduma za usafirishaji wa reli kuanzia leo wakati idadi ya watu waliogoma ikipungua taratibu.

Wakati huo huo shirika hilo la reli limesema matendo yanayoenea ya uharibifu wa mfumo wa reli yameharibu mfumo wa reli kwa treni ziendazo kasi za TGV. Afisa kutoka shirika la reli amesema kuwa matukio kama hayo ya uharibifu yaliyofanyika usiku yamesababisha ucheleweshaji mkubwa kwa huduma za treni ziendazo kasi.