1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haki za binadamu.

Durm, Martin / Straßburg31 Oktoba 2008

Mahakama kuu ya haki za binadamu barani Ulaya yatimiza miaka 10 na bado imethibiti kuwa muhimu katika jukumu la kulinda haki za binadamu.

https://p.dw.com/p/FlF0
Mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya-mjini Straßburg.Picha: AP

Mahakama kuu ya Ulaya inayoshughulikia haki za binadamu inaadhimisha mwaka wa kumi tokea ianze kazi zake mjini Strassburg. Jukumu la mahakama hiyo ni kuhakikisha kwamba haki za binadamu zinatekelezwa kulingana na mwongozo mmoja katika nchi zote za Ulaya.

Yumkini mahakimu 47 wa mahakama kuu hiyo ya Ulaya ya mjini Strasburg hawakupata wasaa wa kukata keki kusherehekea miaka kumi tokea kuwapo kwa mahakama hiyo,lakini hakika wanastahili kupata wasaa wa kufanya hivyo kwani wao ndiyo walinzi wa haki.

Kila mwaka mahakama hiyo inatoa hukumu 1500 zinazohusu kukiukwa haki za binadamu na mashauri yapatayo alfu 80 yanasuburi kushughulikiwa kila mwaka.

Licha ya msongamano wa mashtaka,mahakama hiyo haijatelekeza viwango vya kutoa hukumu.

Watumishi 600 kutoka takriban nchi zote za Ulaya wanafanyakazi kwenye taasisi hiyo yenye ofisi zaidi ya mia nne. Azma ya taasisi hiyo ni kudumisha haki. Kila mwananchi wa nchi 47 wanachama wa mahakama hiyo anayo haki ya kwenda kwenye mahakama hiyo na kudai haki, mradi tu njia nyingine zote za kisheria zimeshindikana katika nchi yake.

Kesi zinazosikilizwa kwenye mahakama hiyo pamoja na zingine zinahusu haki ya mtu kuamua kumaliza maisha yake, juu ya kurutubisha uzazi kwa njia bandia, juu ya masuala ya mali na haki juu ya malezi ya watoto. Mahakama kuu ya Ulaya ya haki za binadamu inafanya kazi ikiwa na fungu la Euro milioni 50 kwa mwakalakini inahitaji fedha zaidi ili kufikia ufanisi mkubwa.

Abdu Mtullya.