1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

030409 Ruanda Genozid

Schulte, Wanjiku8 Aprili 2009

Mwanamuziki Natty Dread adumisha amani kupitia muziki wake

https://p.dw.com/p/HSPw
Mwanamume akiwa Nyamata kusini mwa Kigali akitazama mamia ya mabufuru ya watu waliouwawaPicha: AP

Takriban watu milioni moja waliuwawa wakati wa mauwaji ya halaiki huko Rwanda miaka kumi na tano iliyopita. Baada ya kumalizika mauwaji hayo, wahalifu na wahanga wamauwaji hayo waliwezaje kuishi pamoja kwa amani? Kuweza kuyakubali na kuyasahau walioyaona? Mwanamuziki wa miondoko ya reggea, Natty Dread alikuwa akiishi uhamishoni nchni Ujerumani wakati Wahutu walio wengi walipoanza kuwauwa Watutsi na Wahutu wa msimamo wa wastani. Tukio hilo lilimwathiri sana mwanamuziki huyo. Lakini Natty ameshapata njia ya kukabiliana nalo na kujihusisha na nchi yake.

“Onyesho la kwanza baada ya mauwaji ya halaiki lilikuwa kubwa sana. Watu walikatika na walikuwa na furaha. Hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kuona kwamba watu hawa walikuwa wameshuhudia mauwaji ya halaiki.Uhasama kati ya watu ulikuwa umeisha na kwa hivyo nilijihisi vizuri.”

Natty Dread alifanya onyesho lake la kwanza huko Rwanda miaka miwili baada ya mauwaji ya halaiki. Wakati huo alikuwa pamoja na mamake marehemu Bob Marley na alifanya onyesho lake mjini Kigali mbele ya watazamaji 10,000. Utulivu na furaha iliyokuwepo wakati wa onyesho hilo ilikuwa ya kusisimua.

“Hii ilinipa matumaini na imani kwamba siku za usoni zitakuwa nzuri. Nilimshukuru Mungu nikasema hii ni Rwanda nyingine na Rwanda itakuwa nchi ya kuvutia. Na haya yote yanatendeka hivi sasa. Tuna nchi ndogo lakini nzuri sana”

Natty Dread aliitembelea nchi yake kwa mara ya kwanza na kujionea kwa macho yake mwenyewe yaliokuwa yametokea baada ya mauwaji ya halaiki. Mwanamuziki huyu mwenye umri wa miaka 44 alizaliwa na kulelewa nchi jirani ya Uganda. Mwezi wa April mwaka wa 1994 wakati wanamgambo wa Kihutu, polisi na wanajeshi walipoanza kuwauwa kitatili Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani, Natty alikuwa Ujerumani. Matukio kuhusu mauwaju ya halaiki aliyoyaona katika vyombo vya habari hakuyasahau wakati alipoitembelea Rwanda kwa mara ya kwanza.

“Mwanzoni ilikuwa vigumu sana. Niliona katika runinga jinsi watu walivyokuwa wakikatwakatwa. Hapo hapo nilingiwa na hofu. Nilifikiria wahanga hawa wanaweza kuwa ndugu na dada zangu. Inaweza kuwa mtu yeyote. Nami siwezi kuzuia vitendo hivi. Sikujua lakufanya. Halafu nikawaza vipi watu wanavyojihisi. Hakuna mtu aliyekuwepo kuwasaidia na kuzuia mauwaji haya. Hili lilikuwa jambo la kutisha sana. Kwa muda mrefu nilikuwa na ghadhabu na nilivunjika moyo. Nikafikiria nikikutana na mmoja wa wauwaji hawa, singemuua lakini sikujua ningelimfanya nini!"

Völkermord Friedhof Ruanda
Makaburi nje ya mji wa Kigali nchini RwandaPicha: AP

Watu 18 kutoka kwa familia ya Natty waliuliwa wakati wa mauwaji haya. Hata hivyo amefaulu kukabiliana na chuki na mawazo ya kiubaguzi dhidi ya wauwaji na wafuasi wao nchini Rwanda.

Ujuzi nilioupata huku Ujerumani ulinisaidia, anasema mwanamuziki huyu. Mwanamuziki huyu ameishi mjini Hamburg kwa miaka 20 pamoja na mke wake Myahudi. Mara nyingi walizungumza juu ya mauwaji ya halaiki yaliofanywa dhidi ya wayahudi na kujiuliza kitendo kama hicho kingeweza vipi kutokea. Kwa maoni yake Natty anasema kwamba Wajerumani wametoa mfano mzuri wa kukabiliana na historia yao.

Kukiri makosa yao na kuomba msamaha- hiyo ndio njia sawa katika kufikia amani. Na hili ndilo jambo alilotaka kuwaambia Wanyarwanda alipoitembela nchi hiyo.

“Nilisema labda naweza kuzungumza na watu wangu wa pande zote mbili na kuuliza: Je kuna mtu anayeweza kustahamili ukweli? Kuukubali na kubeba dhamana kwa mambo ambayo wengine waliwatendea wenzao? Halafu tunaweza kutumia uzoefu wa Ujerumani na kuiga sehemu ya historia yao. Mtu angeweza kusema tazama Wajerumani walifanya kitendo kama hiki na sasa wamekubali kosa lao. Kwa nini Wanyaruanda waliofanya mauewaji hayo wasifanye hivyo? Naamini tunaweza kujifunza mengi kutoka Ujerumani: jinsi ya kukabiliana na mzozo. Waliofanya uhalifu huu walikuwa manazi wa Rwanda.”

Natty ni moja kati ya vijana wengi wa kinyarwanda waliokuwa wakiishi uhamishoni wanaorudi nchini kwasababu wanaamini mwanzo mpya baada ya mauwaji ya halaiki.

Kila moja anajaribu katika njia yake tofauti kusaidia kuijenga upya nchi hii. Natty anafanya hivyo kwa kutumia muziki. Wimbo wake maarufu wa kwanza uliochezwa huko Rwanda unazungumzia juu ya watu hawa wanaorudi nchini.

“Habari Rwanda, Kutoka Uganda na kila mahali ninaeleza historia hii kwamba watu Wanyrwanda lazima wapiganie uhuru".

Nchi za magharibi hazikufanya juhudi nyingi kuzuia mauaji hao ya halaiki ya Rwanda yaliyodumu kwa siku 100.