1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani inapaswa kuongoza barani Ulaya

2 Oktoba 2015

.Huu ni mwaka wa 25 tangu nchi mbili za kijerumani ziungane tena. Lakini jee Ujerumani imekubali kulibeba jukumu la kuongoza barani Ulaya.?

https://p.dw.com/p/1Ghl2
Picha: Imago/S. Simon

Mfanyakazi kwenye jopo la wataalamu la mtandao unaoshughulikia migogoro mjini Brussels Sasha de Wijs amesema Ujerumani bado inasuasua katika kulichukua jukumu la kuongoza barani Ulaya, miaka 25 tangu kuungana kwa nchi mbili za Kijerumani.

Mnamo mwaka wa 2013 jarida la Uingereza "The Economist" liliandika kwamba Ujerumani ni dola kuu linalopaswa kuitimiza zaidi dhima ya uongozi barani Ulaya . Na ripota wa gazeti la Ujerumani "taz" Eric Bonse alisema kutokea mjini Brussels kwamba Ulaya ni Ujerumani.

Ripota huyo amefahamisha juu ya ushawishi mkubwa wa Ujerumani katika taasisi za Umoja wa Ulaya kama vile, katika halmashauri, baraza la mawaziri na kwenye bunge la Ulaya.

Ufaransa haina hofu mbele ya Ujerumani

Hata hivyo aliekuwa Waziri wa Ufaransa aliekuwa anayashughulikia masuala ya Umoja wa Ulaya Nolelle Lenoir hakuweza kuubainisha ushawishi mkubwa wa Ujerumani katika Umoja wa Ulaya. Waziri huyo alisema wakati huo kwamba Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ni mwana Ulaya mkubwa kuliko mtu mwengine yeyote

Ni hivi karibuni Waziri Lenoir alisema kuwa Kansela Merkel ni mwanasiasa ambae yuko tayari kufikia mwafaka na kwamba Merkel ni kiongozi anaeyatilia maanani maslahi ya Ufaransa.

Kwa miaka mingi uhusiano baina ya Ujerumani na Ufaransa ndiyo umekuwa nguzo ya Umoja wa Ulaya na injini ya maendeleo.
Hata hivyo kwa sasa Ujerumani ndiyo injini ya kweli ya maendeleo barani Ulaya kutokana na Ufaransa kudhoofika kiuchumi .

Hayo ameyasema mbunge wa Bunge la Ulaya Elmar Brok ambae pia ni mjumbe wa kamati ya masuala ya nje ya Bunge hilo.Bwana Brok tayari alikuwa mbunge wa Ulaya wakati nchi mbili za kijerumani zlipoungana tena miaka 25 iliyiopita.

Bwana Brok ameeleza kwamba Ufaransa inapaswa kuwa na nguvu kubwa za kiuchumi ili kuweza kulibeba jukumu la kuongoza barani Ulaya pamoja na Ujerumani. Lakini amehoji kwamba katika dhima hiyo ya uongozi, Poland pia ni muhimu.

Kutokana na nchi mbili za kijerumani kuungana tena, Ujerumani mashariki ilikuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya moja kwa moja.Hata hivyo wanachama wengine wa Umoja wa Ulaya kama vile Uingereza walikuwa na mashaka juu ya uanachama wa Ujerumani iliyoungana tena. Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani walijishtukia kuwa wanachama wa Umoja wa Ulaya mara tu baada ya Ujerumani kuungana tena.

Feier zur Deutschen Einheit in Berlin
Picha: picture-alliance/dpa

Hapakuwapo ulazima wa kufanyika mazungumzo marefu wala pilikapilika kubwa za kisheria . Mazungumzo yalianza mapema mnamo mwaka wa 1990 na hadi kufikia mwezi wa Juni, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani iliingizwa katika Umoja wa Ulaya.

Na mnamo mwaka huo huo mchakato wa kuunda umoja wa sarafu ulianzishwa kwenye mkutano wa kilele wa viongozi wa Ulaya uliofanyika katika mji wa Ireland, wa Dublin.

Na kuhusu migogoro ya sasa ya Ugiriki na wakimbizi Ujerumani inatimiza dhima ya uongozi. Na hasa juu ya masuala ya kiuchumi na nidhamu ya bajeti Ujerumani ni mnyapara anaeonekana na kiboko mkononi.

Mwandishi:Riegert Bernd.

Mfasiri:Mtullya Abdu.

Mhariri:Josephat Charo