1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 47 ya Mapinduzi, Zanzibar

12 Januari 2011

Leo msikilizaji imetimia miaka 47 tangu kutokea kwa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yalioiangusha serikali ya Sultan ilioongozwa na Waziri mkuu Mohamed Shamte Hamadi.

https://p.dw.com/p/zwnQ
Rais wa Zanzibar, Dokta Ali Mohamed SheinPicha: DW

Itakumbukwa kwamba karibu miezi minne baadae, Zanzibar ikaungana na iliokuwa Tanganyika  kuunda  ile inayoitwa hivi sasa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sikiliza mahojiano kati ya Halima Nyanza na Profesa Abdul Sharrif, mchambuzi wa masuala ya historia na siasa, visiwani humo na kwanza  anaelezea maoni yake juu ya umuhimu wa mapinduzi hayo.

Mwandishi: Halima Nyanza Mhariri: Mohammed Abdulrahman