1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MIAKA 50 UMOJA WA ULAYA

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFq

TAARIFA YA HABARI 24-03-07 11.000

BERLIN:

Viongozi wa dola na serikali wa Umoja wa Ulaya wanakusanyika leo mjini Berlin,Ujerumani kuadhimisha mwaka wa 50 tangu kutiwa saini Mkataba wa Roma, ulioweka jiwe la msingi la Umoja wa Ulaya. Kilele cha sherehe hizi ni kutiwa saini kwa taarifa inayotetea desturi za pamoja za nchi za Ulaya na shabaha za siku zijazo-taarifa ambayo itajulikana kama „Tangazo la Berlin“.

Taarifa hii haitahusika kwa aina yoyote na katiba ya Umoja wa Ulaya ambayo ilikataliwa miaka 2 iliopita katika kura za maoni na wafaransa na Waholanzi.

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani amefanya kuifufua katiba hiyo kuwa mojawapo ya shabaha zake kuu katika kipindi chake cha miezi 6 kama rais wa UU.