1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miami, Marekani. Noriega akataliwa kurejea kwao baada ya kifungo.

25 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWH

Jaji wa mahakama nchini Marekani jana Ijumaa ametupilia mbali madai ya rais wa zamani wa Panama Manuel Noriega kutaka arejeshwe haraka nchini kwake baada ya muda wa kifungo nchini Marekani utakapomalizika mwezi ujao na kusema kuwa hakuna kikwazo dhidi ya ombi la Ufaransa kumpeleka nchini humo.

Wakili wa Noriega amedai mahakamani kuwa hadhi ya mteja wake kama mfungwa wa kivita baada ya kukamatwa wakati wa uvamizi wa majeshi ya Marekani nchini Panama zaidi ya miaka 17 iliyopita inampa fursa ya kurejeshwa mara moja baada ya kuachiliwa kwake huru kutoka jela ya Florida hapo Septemba 9.

Lakini jaji kiongozi William Hoeveler amesema Noriega aliepata hadhi hiyo kutokana na mkataba wa Geneva akiwa kama mfungwa wa kivita , hauzuwii kupelekwa katika nchi ya tatu kama Ufaransa, ambako anakabiliwa na adhabu ya kifungo ya miaka 10 kutokana na madai ya kupeleka fedha za biashara ya madawa ya kulevywa.