1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michezo: matokeo mwishoni mwa Juma.

Mohammed AbdulRahman27 Novemba 2006

Ligi kuu ya kandanda nchini Ujerumani Bundesliga sasa yazusha mchuano mkali ,matokeo ya kombe la Afrika mashariki na kati , mashindano yanayofanyika huko Ethiopia na bondia Axel Schulz ashindwa kutamba mbeleya Mmarekani Brian Minto-karibu.

https://p.dw.com/p/CHct
Rafinha kutoka Brazil akisherehekea bao lake lililokua la kwanza katika ushindi wa Schalke wa mabao 3-1 dhidi ya Bochum
Rafinha kutoka Brazil akisherehekea bao lake lililokua la kwanza katika ushindi wa Schalke wa mabao 3-1 dhidi ya BochumPicha: AP

Kandanda : Schalke 04 bado inaendeleakuongoza katika ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga,baada ya kufanikiwa katika uwanja nyumbani kuwabwaga wageni wao Bochum mabao 2-1. Ama mpambano wa kusisimua mwishoni mwa juma ulikua ni ule kati ya miamba ya kaskazini Hamburg na wa kusini Bayern Munich. Hamburg ilishindwa kuwika nyumbani na kujikuta ikizidi kudidimia katika janga la hatari ya kushuka daraja ilipofungwa mabao 2-1 na Bayern Munich. Katika hatari hiyo ya kuteremka daraja, Hamburg inaungana na Bochum na Mainz, iliorudi nyumbani ikiwa imelala bao1-0 mbele ya Hannover.

Kwa ushindi wake huo Bayern ambao ndiyo mabingwa watetezi sasa inachuana vikali na Schalke na Werder Bremen katika kinyangayiro hicho cha ubingwa msimu huu. Timu nyengine ni Stuttgart Borussia Monchengladbach 1-0 na sasa inashika nafasi ya tatuKatika msimamo jumla wa Bundesliga Schalke inaongoza kwa pointi 29, ikifuatiwa na Bremen ikiwa na pointi 27 baada ya ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Armenia Bielefeld, Bayern ina poniti 26 na iko nafasi ya nne nyuma ya Stuttgart

Katika orodha ya wafungaji mabao mengi hadi sasa katika ligi kuu ya Ujerumani, anayeongoza ni Pantelic wa Hertha Berlin aliyeuona wavu mara 9, wakati RoyMakaay wa Bayern Munich , Gomez wa Stuttgart na Miroslav Klose wa Werder Bremen wana magoli 8 kila mmoja.

Mashindano ya kuwania kombe la Afrika mashariki na kati Challenge Cup yalianza mwishoni mwa juma , huku Ethiopia ambayo ni mwenyeji wa mashindano ikiutetea ubingwa wake. Itakumbukwa Ethiopia ililinyakua kombe hilo ilipoilaza Burundi 3-0 katika fainali ya mwakajana. Katika pambano la fungua dimba dhidi ya hata Ethiopia ilishindwa kuwika ilipokandikwa na Tanzania bara 2-1 na Malawi ikailaza Djibuti 3-0.

Katika patashika ya ligi kuu ya Uingereza Premier League, mechi iliokua ikisubiriwa kwa hamu kati ya Manchester United na Chelsea jana ,sare ya 1-1, matokeo yalioibakisha pia Manchester katika uongozii kiwa na pointi 3 zaidi ya mabingwa watetezi Chelsea. MANU ina jumla ya pointi 34. Ama Arsenal ya mjini London maarufu kama Gunners walishindwa kaumini pale mchezaji wao wa zamani Anelka alipotingisha wavu mara mbili, kuongeza ushindi wa timu yake ya Bolton Wanderers wa mabao 3-I. Katika pambano jengine bao pekee la mchezo lililofungwa na Steven Gerrad liliipa ushindi Liverpool dhidi ya Manchester City.

Wakati huo huo Mshambuliaji hatari wa Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney amerefushiwa miaka miwili zaidi katika mkataba wake na MANU hadi 2012. Kutokana na mkataba wake mpya sasa Ronney atajikingia kitita cha pauni 150,000 kwa wiki.

Nchini Uhispania Barcelona, ilihakikisha inajizatiti kwenye kiti cha uongozi ilipoipa funzo Villareal la mabao 4-0. Barca sasa wakiwa na pointi 29 wako pointi 1 tu zaidi ya wapinzani wao wakubwa Sevilla inayofuatwa na Real Madrid yenye pointi 26.

Ubondia: Bondia wa Ujerumani wa uzito wa juu Axel Schultz amegonga mwamba katika juhudi yake ya kutaka kuruditena ulingoni. Schultz mwenye umri wa miaka 38, alijikuta akipigwa na Mmarekani Brian Minto aliyemaliza udhia katika raundi ya 6. Shultz alianguka kwanza aliposhambuliwa kwa masumbwi makali katikad duru ya nne, lakini akaendelea hadi aliposhindwa kabisa baada ya dakika 1 na sekunde 30 ya duru ya 6.Ulikua ni ushindi wa 27 kwa Minto katika jumla yamapambano yake 28.