1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michezo mwishoni mwa wiki

4 Aprili 2008

Hongo katika dimba la uingereza ? Mwenge wa Olimpik kuptia Dar-es-salaam

https://p.dw.com/p/DcI7
Schalke:Jermaine JonesPicha: AP

Mji wa Dar-es-salaam ukijiandaa kama mji pekee wa Afrika kupokea mwenge wa olimpik ukiwa njiani kuelekea Beijing, klabu za Ulaya zinajiwinda kurudi uwanjani mwishoni mwa wiki hii kwa kinyan'ganyiro cha vikombe vya Ligi:

Viongozi wa ligi ya ujerumani Bayern munich wana matumaini ya kubakia muda mrefu kileleni licha ya kumudu suluhu tu ya bao 1:1 katika kombe la ulaya la UEFA na Getafe ya Spian.

Wakati Rio ferdinnand anakaribia kurefusha mkataba wake na Manchester united na Ronaldinho amerudi uwanjani kwa mazowezi na Barcelona,Premier League-ligi ya Uingereza ina kashfa mpya: Mchezaji wake mmoja amepokea hongo la dala laki 1 kuachia timu yake kushindwa.

Tuanze na Bundesliga-Ligi ya Ujerumani:Munich iliofungua mwanya wa pointi 7 kileleni watapiga hatua nyengine kukaribia taji lao la 21 wakiitimua kesho jumapili Bochum.

Bochum imekua ikichchachamaa hivi karibuni na Munich inatambua hayo.Hamburg iliopo nafasi ya pili ya ngazi ya Ligi ina miadi leo na mabingwa wa Ujerumani-Stuttgart.Na bila ya wachezaji wake 2 maarufu David Jarolim na Joris Mathijsen walioumia.stuttgart imekua ikijitutumua karibuni hasa kwa kuwika jogoo lao Mario Gomez.

Hamburg yajivunia Mohamed Zidan wa Misri alietamba katika kombe la Afrika la mataifa huko Ghana hapo Februari.

Schalke 04 wanatetea nafasi yao ya 3 nyuma ya Hamburg na munich wakicheza leo na Hansa Rostock.Pigo walilopata Schalke la bao 1:0 kutoka kwa Barcelona katika champions League kati ya wiki hii limewaachia majonzi ya pengine kuaga karibuni kombe hilo.kwahivyo wana kila sababu ya kutamba leo.soren Larsen huenda akampokonya Kevin Kuranyi nafasi yake usoni alao kwa muda.

Borussia Dortmund ina miadi kesho na Bayer Leverkusen.

Katika changamoto za kombe la FA -Uingereza ambako premier League-imegubikwa na kashfa mpya ya hongo,

West bromwich Albion wana miadi jumamosi hii na Portsmouth.

Sir Alex Ferguson ,kocha wa Manchester united amefichua kwamba beki wao mshahara Rio Ferdinand alieiongoza england katika mpambano na Ufaransa mwezi uliopita mjini Paris,atarefusha mkataba wake na M ANU.Mlinzi huyo wa zamani wa West ham na Leeds ,amebakisha miezi 14 kukamilisha mkataba wake wa sasa na MANU na inatumai atabakia.

MANU inafunga safari leo kucheza na Middlesbrough ili kuseleleza kileleni uongozi wake wa premier League.

Chama cha mpira cha Uingereza FA kimearifu jana kwamba kinachungua tuhuma kwamba mchezaji wa zamani wa premier League amepokea kitita cha dala 100 kama mrungura kugeuza matokeo.Mchezaji huyo ambae hakutajwa alicheza ngware makussudi ili atolewe nje ya uwanja katika mechi iliochezwa Uingereza mnamo miaka 2 iliopita.Kisa hiki kilifichuliwa jana na gazeti la Independent.

Huko Spain la Liga, pia inarudi uwanjani na stadi wa Brazil Ronalindinho ameanza mazowezi na wenzake. Huenda akateremshwa uwanjani baada ya kuweka nje ya chaki kwa wiki 3.Barcelona inateremka kesho uwanjani wakati mahasimu wao Real Madrid wana miadi na Real Mallorca.

Mwishoe, Dares-salaam ni mji pekee wa Afrika ambako mwenge wa olimpik ulioondoka Ugiriki wiki iliopita utapita kuelekea Beijing.Mwenge huo utakaowasili dar kutoka Buenos Ares,Argentina hapo April 12,utapokewa Dar kwa shangwe na shamra shamra.

kikosi cha watanzania 71 kimechaguliwa pamoja nao wanariadha wa zamani kama Bingwa wa rekodi ya dunia ya mita 1500 Philbert Bayi na mshindi wa medali ya fedha wa olimpik Suleiman Nyambui.Hata waziri wa maswali ya muungano Mohammed Khatib atajiunga na mwenge huo.