1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michezo mwishoni mwa wiki

4 Januari 2010

Kombe la Afrika la Mataifa Angola

https://p.dw.com/p/LKvA
VfL Wolfsburg - wako Afrika Kusini.Picha: picture-alliance/ dpa

Wiki kabla Kombe la Afrika la Mataifa kuanza nchini Angola Jumapili ijayo, tunawafungulia pazia jinsi ya baadhi ya timu 16 pamoja na wenyeji Angola, zilivyojiwinda kuivua taji Misri, mabingwa.Mabingwa wa Ujerumani VFL Wolfsburg, wamewasili Afrika Kusini kwa mazowezi ya siku 3 kabla ya kuanza duru ya pili ya Bundesliga .Na Manchester United inaaibishwa na chipukizi Leeds United na kupigwa kumbo nje ya Kombe la kutoana la FA.

Bundesliga na Premier League:

Mabingwa wa Ujerumani, VFL Wolfsburg, ambao hawakuanza uzuri duru ya kwanza ya msimu,wameamua kupiga kambi kwa mazowezi ya siku 3 nchini Afrika Kusini-kituo cha kombe lijalo la dunia hapo Juni 11-Julai 11.Wolfsburg kwahivyo, imekuwa timu ya kwanza ya Bundesliga,kupiga kambi Afrika kusini,mwenyeji wa kombe la dunia.Mabingwa hawa wa Ujerumani , wanacheza jioni hii na mabingwa wa kombe la washindi la Afrika kusini, Moroka swallows.Timu zote mbili, Wolfsburg na Moroka zina mfadhili mmoja:Kiwanda cha magari cha Volkswagen .Isitoshe, Moroka Swallow ina kocha mjerumani, Rainer Zobel.

Ziara hii ya mabingwa wa Ujerumani, itachangia kuzijaribu zana za kufanyiwa mazowezi kwa timu za dimba za kombe la dunia za chuo kikuu cha Nelson Mandela Metropolitan University, kiwanja ambacho kimetengwa rasmi kwa mazowezi ya timu za Kombe la dunia linaloanza kuanzia Juni 11 hadi Julai 11 mwaka huu.Mji wa Port Elizabeth,utaandaa jumla ya mapambano 8 ya kombe la dunia.

Wolfsburg, ilishinda kwa msangao wa mashabiki wengi taji la Bundesliga mwaka jana ikitamba na majogoo wake 2:mbrazil Grafite na mbosnia Edin Dzeko ambao kwa pamoja, walitia msimu uliopita si chini ya mabao 50.Tangu kuanza duru ya kwanza ya msimu huu, Wolfsburg chini ya kocha mpya,wamekuwa wakipepesuka na wameangukia nafasi ya 8 ya ngazi ya Ligi.

Bundesliga, itarudi uwanjani baada ya likizo ya X-masi na mwaka mpya kati ya mwezi huu.Majogoo wake wengi wa kiafrika, watakuwa Angola kwa kombe la Afrika la Mataifa linaloanza Januari 11.

KOMBE LA FA UINGEREZA:

Premier League-Ligi ya Uingereza, ilipumzika ili kutoa nafasi kwa kinyan'ganyiro cha Kombe la FA :Manchester United,iliopo nafasi ya pili ya ngazi ya Premier League,

ilipata pigo lake kali kabisa tangu miaka 26 ilipopigwa kumbo hapo jana nje ya Kombe la FA na Leeds United .Bao la dakika ya 19 la mshambulizi Jermaine Beckford ,liliitoa Manu katika duru ya 3 kwa mara ya kwanza tangu ilipokiona cha mtema kuni kutoka Bournemouth, 1984.Pia ni mara ya kwanza kwa Sir Alex Ferguson, kocha wa Manu kuaibishwa namna hivyo katika duru ya 3 ya kombe la FA.itakua asie na mwana aeleke jiweSasa kura mepigwa kwa duru ya 4 ya Kombe hili la FA.Leeds United ,walioiteka Manu watakuwa na changamoto nyengine na Tottenham Hotspurs.Chelsea, viongozi wa Premier League, wana miadi na Preston North wakati Wolverhampton Wanderers watawakaribisha Crystal Palace.

Kombe la Afrika la Mataifa :

Jumapili ijayo,Januari 10 hadi 31 itakua " asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo-mkutano nchini Angola." Misri, au mafiraouni kama timu ya Taifa inavyofahamika, wataingia uwanjani kutetea taji lao walilolitwa miaka 2 iliopita nyumbani Cairo, walipoitoa kwa bao 1:0 Ivory Coast.Misri, imeangukia kundi C pamoja na Nigeria,Benin na Msumbiji.Kocha wa Misri,

Hassan Shehata, ameteua kikosi chake tayari na miongoni mwa mastadi wengine, yum,o kipa Essam Al-haidari kutoka klabu ya nyumbani ya Ismailia,wachezaji wa kiungo Ahmed Hassan na mwenzake Hosni Abd Rabou wa (Al Ahli,Misri ) na Ahli-Dubai).kikosi cha mabingwa kinajumuisha pia washambulizi hatari kama vile Mohamed Zidan wa klabu ya Bundesliga ya Borussia Dortmund na Ahmed Eid.Je, Miri itawika tena au Tembo wa ivory Coast wakiongozwa na nahodha wao kutoka Chelsea, Didier Drogba watawavua taji ?

Kwavile, Ivory Coast, ndio timu inayopigiwa sana upatu kutamba katika Kombe lijalo la dunia huko Afrika Kusini, itakodolewa sana macho iwapo sio tu italipiza kisasi kwa Misri kwa kulazwa katika finali iliopita au pia itatoroka na taji ili kutilia nguvu matarajio makubwa inayowekewa katika Kombe la dunia.

Ikijumisha mastadi kama mlinzi Kolo Toure wa Manchester City na Guy Demel wa Hamburg , mastadi wa kiungo Yaya Toure wa FC Barcelona na washambulizi Didier Drogba na Salomon Kalou wa Chelsea, Tembo wa Ivory Coast, ni wazito vya kutosha kuwakanyaga maadui zao na kutamba porini Angola.Na ili kujiweka tayari kwa zahama za wiki ijayo huko Angola, Tembo wanaingia uwanjani jioni hii mjini Dar-es-salaam kupimana nguvu na Kilimanjaro Stars, timu ya taifa ya Tanzania na baadae Ruanda. Je, vipi matumaini ya wenyeji Angola, waliotia fora sana tangu katika Kombe lililopita la Afrika la Mataifa na hata Kombe la dunia hapa Ujerumani ?

Wenyeji Angola, wanadai "mcheza kwao hutunzwa",lakini ni jana tu walipomudu sare tu ya bao 1:1 na Gambia katika mpambano wao wa mwisho wa kujiandaa kwa Kombe hili la Afrika.Ni Angola itakayofungua dimba Jumapili ijayo na Mali mjini Luanda.Ilikua Gambia, iliolifumania kwanza lango la Angola dakika ya 4 ya mchezo kwa bao la Ebrima Sawaneh kabla stadi wao Manucho, mshambulizi wa zamani wa Manchester United, anaesakata sasa dimba nchini Spain, kusawazisha mnamo dakika ya 29 ya mchezo.

Timu nyengine inayo kodolewa macho kutamba katika Kombe hili ni Ghana (Black Stars).Kabla kuanza Kombe hili,nahodha wao amebidi kuteremka melini-John Mensah,kipa wa taifa ameumia wakati klabu yake ya Sunderland ilipocheza katika Pemier League hivi karibuni.Hata mlinzi wao John Painstil, atakuwa nje ya chaki ya uwanja baada ya kuumia goti akiichezea Fulham,mwishoni mwa wiki iliopita.Ghana, imemuita Jonathan Mensah, kujaza pengo langoni wakati nafasi ya painstil itajazwa na Ransford Osei wa Getafe ya Spain.

Ghana imeangukia kundi B na maadui zao si wengine bali Tembo wa Ivory Coast,jirani zao,Burkina Faso na majirani wengine Togo. Wakiongozwa na stadi wao wa kiungo Michael Essien wa Chelsea,Ghana inatumai washambulizo wake akina Kwadowo Asamoah na Asamoah Gyan watatamba mbele ya Ivory Coast na mwishoe Togo.

Timu nyengine ya kuogopwa ni Nigeria ambayo ilipatwa na msukosuko wa kumuuguza mshambulizi wao wa Bundesliga-Obafami Martin wa mabingwa VFL Wolfsburg .Martin, amekuwa akikaguliwa na madaktari huko Durban ili kujua iwapo amepona sawa sawa kwa changamoto za wiki ijayo.Ikiwa si fit, basi mshambulizi mwengine wa Bundesliga, Chinedu Obasi, wa klabu ya Hoffenheim,atajaza pengo lake.Nigeria, iliokata tiketi ya kombe la dunia , ina miadi ikiangukia kundi moja na Msumbiji,Benin na mabingwa Misri.Mpambano wake na Misri, utaamua hatahivyo, hatima ya Nigeria.

Mwandishi: Ramadhan Ali/ RTRE/DPAE

Uhariri: Othman Miraji