1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michezo ya Olympic ya Beijing

Hamidou, Oumilkher23 Agosti 2008

Kenya yatamba na kunyakua medali mbili za dhahabu hii leo

https://p.dw.com/p/F3bw

Na hatimae katika michezo ya Olympic ya Beijing,leo ilikua siku ya Kenya kutamba.Wilfried Bungei alinyakua dhahabu katika mbio za mita 800,mwenzake Alfred Kirwa Yego (bingwa wa dunia wa masafa hayo) akanyakua shaba.Medali nyengine ya dhahabu ya Kenya imeletwa leo na Nancy Langat katika mbio za mita 1500 wanawake.Katika mbio za mita elfu tano wanaume,Kenya ililazimika kuridhika na medali za fedha na shaba,ushindi ukimwendeya bingwa wa Olmpics wa masafa hayo Kenenisa Bekele wa Ethiopia,aliyeigiza ushindi kama huo katika mbio za mita elfu kumi na mita elfu tano wa msichana Tirunesh Dibaba wa Ethiopia.