1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano ya kombe la mataifa ya ulaya

Mohammed AbdulRahman18 Oktoba 2007

Rumania, Jamhuri ya Cheki na Ugiriki nazo zakata tiketi ya fainali za 2008, lakini England yaacha masuali .

https://p.dw.com/p/C7nI
Libor Sionko wa Jamhuri ya Cheki akisherehekea bao la kwanza katika ushindi wa timu yake wa 3-0 dhidi ya Ujerumani.
Libor Sionko wa Jamhuri ya Cheki akisherehekea bao la kwanza katika ushindi wa timu yake wa 3-0 dhidi ya Ujerumani.Picha: AP

Rumania ,Jamhuri ya Cheki na mabingwa watetezi wa kombe hilo Ugriki sasa zimejiunga na Ujerumani iliokata tiketi ya fainali hizo tangu wiki iliopita, baada ya Rumania kuilaza Luxembourg mabao 2-0 na Ugiriki iliokua pia ikicheza ugenini kuwatandika majirani zao Uturuki bao 1-0.

Ujerumani licha ya kufanikiwa, ilipata pigo katika uwanja wa nyumbani mjini Munich ilipokandikwa mabao 3-0 na Jamhuri ya Cheki na kuwaacha mashabiki wake wakipigwa na bumbuwazi.

Pamoja na kushindwa , akizungumzia mchezo huo dhidi ya Cheki.

Jamhuri ya Cheki imejiweka nafasi nzuri pia ya kufanikiwa kwani pamoja na Ujerumani zote zimecheza mechi 10 na zina pointi 23 kila moja.

Kwa upande wake England imejiweka pabaya katika jitihada za kutaka kufunzu na kucheza fainali hizo baada ya kufungwa na Russia mjini Mosko mabao 2-1. Wakati England ilipokua ikiongoza kwa bao lililofungwa na Wayne Rooneyhatua ya muamuzi Luis Medina Cantalejo kuipa Urusi mkwaju wa Penalty baada ya Rooney kumvuta Kostaantin Zyryanov, ulionekana kuwa uamuzi usio sahihi kwani kitendo hicho kilikua dhahiri nje ya eneo la adhabu hiyo.

Kabla ya England haijakaa sawa bao jengine likaizamisha kabisa, na sasa kunusurika kwake kutategemea matokeo ya mechi mbili za Urusi dhidi ya Andora na Israel. Ikiwa Urusi itashinda mech zote basi England itayaaga mashindano ya mwakani.

Ufaransa nayo imepiga hatua mbele na kujiwekea matumaini na kushika nuongozi wa kundi linalozijumuuisha pia Scotland na Italia. Wakati Ufaransa iliibwaga Lithuania mabao 2-0, Scotland iliokua ikiongoza kundi hilo, ilipata pigo baada ya kufungwa na Georgia mabao 2-0 wakati ilikua ikihitaji pointi 4 tu katika michezo yake miwili kukata tiketi ya fainali hizo. Kwa upande wa Ufaransa mabao yote mawili yalifungwa na Thierry Henry na kuvunja rekodi ya mchezaji wa zamani aliyewahi kuwa nahodha wa timu ya Ufaransa na mchezaji bora wa Ulaya Michel Platini ya magoli 41.

Henry mwenye umri wa miaka 30 ,sasa amefunga jumla ya mabao 43 katika mechi 96 alizocheza akiwa katika timu ya taifa.

Timu mbili za kwanza katika kila kundi ndizo zitakazocheza fainali za kombe la mataifa ya ulaya 2008.

Nje ya michuano hiyo ya kandanda ya kombe la mataifa ya ulaya, kesho timu ya Rugby ya Ufaransa mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia yanayofanyika nchini humo itachuana na Argentina kutafuta mshindi wa tatu baada ya timu hizo ku´ngolewa katika nusu fainali. Ufaransa ilifungwa na watetezi wa kombe hilo Uingereza na Argentina ikalazwa na Afrika kusini.

Fainali kati ya England na Afrika kusini inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mchezo huo, na itakayokua ya Asiye na Mwana aeleke Jiwe na Asiye na mguu atiye Gongo, itachezwa mjini Paris Jumamosi.